Wakati wa utawala wa ukoloni barani Afrika, maelfu ya vinyago viliharibiwa. Nchi za Afrika zinataka virudi na makavazi makubwa zaidi kote ulaya yamekubali kutoa vinyago maarufu vya shaba vya Benin kwa mkopo kwenda Nigeria.
Sasa Ufaransa inazindua ripoti ya kutoa wito wa kutaka maelfu vinyango kutoka Afrika vilivyo kwenye makavazi yake kurudishwa Afrika.
Shaba za Benin

Shaba za Benin ni mkusanyiko wa vinyago vya thamani kubwa vilivyokuwa kwenye kasri la kifalme la Oba, Ovonramwen Nogbaisi, katika ufalme wa Benin.
Vilichongwa kutoka kwa pembe za ndovu, shaba na kutoka kwa miti.
Vingi vilichongwa kwa madhabahu ya wafalme za zamani na malkia.
Mwaka 1897 Waingereza waliendesha uvamizi dhidi ya Benin kujibu shambulizi dhidi ya wanadiplomasia wa Uingereza.
Kando na vinyago vya shaba, vifaa vingi vilichukuliwa na sasa vinasambazwa kote duniani.

Makavazi mjini London yanasema kuwa vifaa kutoka Benin viliwasilishwa kwake mwaka 1898 na ofisi ya mashauri ya nchi za kigeni.
Mwezi Oktoba makavazi makubwa ya barani Ulya yalikubali kutoa kwa mkopo vinyago kwenda nchini Nigeria kwa makavazi yake mapya yanayopangwa kufuguliwa mwaka 2021.
Simba wala watu

Hawa ni simba wawili maarufu wala watu kutoka eneo la Tsavo nchini Kenya, Afrika Mashariki ambao waliwaua na na kuwala wafanyikazi wa reli kutoka nchini Uingereza waliokuwa na asili ya Kenya -Uganda mwishoni mwa karne ya 19
Wafanyikazi hao walikuwa wakijenga reli kati ya Mombasa na ziwa Victoria kwa miezi tisa mnamo mwaka 1898.

Simba hao walipigwa risasi na kuawa na mhandisi wa Ungereza Luteni kanali John Patterson.
Sanamu ya simba hao ilinunuliwa kutoka kwa Patterson na makavazi ya historia ya Marekani iliyopo mji wa mwaka 1925 na kuhifadhiwa kama vituo asilia vya kudumu.
Luteni kanali Patterson aliripoti kuwa simba hao waliwaua na kuwala takribani wafanyikazi 135 wakiwemo waafrika weusi, Lakini makavazi inayohifadhi mabaki yao baadaye ilisema watu waliouawa walikuwa karibu 35.
Hayo ni kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi wao.
Makavazi ya kitaifa ya Kenya sasa inataka mabaki ya simba hao kurejeshwa nyumbani.
Jiwe la Rosetta

Jiwe hilo la Rosetta la urefu wa mita 1.12 kwenye makavazi ya Uingereza likitokea nchini Misri.
Ni sehemu ya jiwe kubwa lenye maandishi juu yake ambayo yamewasaidia watafiti kujifunza jinsi kusoma kuhusu mifumo ya kuandika nchini Misri uliotumia picha na ishara.
Haijulikani vile jiwe hilo liligunduliwa mwezi Julai mwaka 1799 lakini kuna imani kuwa liliguduliwa na wanajeshi waliopigana na kiongozi wa jeshi la Ufaransa Napoleone Bonaparte wakati wakijenga kwenye mji wa Rashid.
Wakati wa Napoleon, Waingereza walichukua umiliki wa jiwe hilo chini ya makubaliano yaliyofahamika kama Treaty of Alexandria mwaka 1801.
Malkia Bangwa

Hii ni sanamu maarufu la kuchongwa la Malkia Bagwa kutoka inayojulikana sasa kama Cameroon mwishoni mwa karne ya 19.
Sanamu hilo lenye urefu wa inchi 32 au (sentimita 81) linaashiria madaraka na afya ya watu wa Bangwatall Bangwa.
Ni moja ya sanamu maarufu zaidi Afrika na ina umuhimu mkubwa kwa watu nchini Cameroon.
Sanamu zilichongwa na kupewa majina ya wake wa wafalme au wanaufalme na kuitwa Malkia wa Bangwa huko Bangwa.
Sanamu ya Malkia wa Bangwa labda ilipewa au kuibwa na wakoloni wa Ujerumani karibu mwaka 1899 kabla ya eneo hilo kutawaliwa na wakoloni.
Vito vya thamani vya Maqdala

Vito vya thamani ya Maqdala ni pamoja na taji la karne ya 18 na nguo ya harusi vilivyochukuliwa kutoka Ethiopia na jeshi la Uingereza mwaka 1868.
Wanahistoria wanasema ndovu 15 walihitajika kubeba vifaa vilivyoibwa kutoka Maqdala.
Waingereza walivamia Maqdala kupignha kutwalia kwa ubalozoi wao wakati uhusiano kati ya pande hizo ulidorora.

Ndege wa Zimbabwe

Vinyago nane wa ndege wa Zimbabwe waliibwa kutoka mahame ya mji wa zamani.
Ni ndege nane waligunduliwa. Walikuwa kwennye kuta za mji wa kale uliojengwa kati ya karne ya 12 na 15 na wahenga wa watu wa Shona.
Saba kati ya vinyago hao walikuwa nchini Zimbabwe tangu mwaka 2003 wakati mmoja alirudishwa kutoka Ujerumani.
0 Comments