HISTORIA YA WABENA





ASILI YA KABILA LA WABENA

Kwa sasa Wabena ni moja ya kabila linalopatikana katika mkoa wa Iringa na Njombe. Ni moja ya kabila ambalo lugha yake ina utajiri wa maneno, lugha hiyo inaitwa kibena.

Historia inafahamika kuwa makabila mengi ya kibantu hapo mwanzoni hayakuwa katika makundi ambayo yaliwatambulish
a kama kabila. Bali Wabantu walikuja wakiwa kwenye makundi yaliyokuwa katika ngazi ya Ukoo. Na hii ilitokea hata kwenye kabila la Wabena.

Wabena ni moja ya kabila ambalo lilijiwekea historia kubwa hasa pale kwenye vita kati ya Wakamba na Wazaramo kwenye miaka ya 1750. Mwanzoni kabisa kabila hili halikufahamika kama Wabena. Wabena walipata kuishi wakiwa na mahusiano mazuri na kabila la Wazaramo.

Historia ya Wabena inafafanuliwa kwa ufupi kuwa, kabla ya kabila hili kuwa katika ngazi ya kabila lilikuwa katika ngazi ya ukoo. Ukoo huo uliitwa Wang’hoo. Na ukoo huu ulipata kujulikana na Wazaramo na uli pendwa sana. Ukoo huu ulikuwa ukijihusisha sana na biashara zilizokuwa zikifanywa maeneo ya mwambao ambapo Washomvi walikuwa wenyejii.

Kulitokea wakati kuliingia watu kutoka katika ardhi ya Ukamba yaani Wakamba. Watu hao walivamia maeneo ya pwana na kufanya vurugu kwa Wazaramo na wenyeji wengine waliokuwa wakiishi kwenye maeneo hayo. Wakati huo Wakamba wakiingia kwenye ardhi ya Wazaramo, kulikuwa na Shujaa wa kizaramo aliyejulikana kwa jina la Bwana Pazi Kilama aliyekuwa akiishi maeneo ya Kinyangulu.

Kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikifanywa na Wakamba, baadhi ya wenyeji pamoja na Wafanyabiasharawa Kibena huko mwambao waliomba msaada kwa Shujaa pazi. Na kutokana na uwezo aliokuwa nao shujaa huyo, aliamua kwenda kuwapiga Wakamba. Lakini kabla ya kwenda kwenye vita hivyo na wakamba, Shujaa Pazi Kilama, alikusanya jeshi lake.

Miongoni mwa wanajeshi walitoka kwenye ukoo wa Wang’hoo. Na kutokana na uhimara wao, walipigana kwa nguvu zote na kuwapiga Wakamba wote na kuwafukuza. Na mara baada ya vita kuisha, inasemekana kuwa Wang’hoo waliamua kuwa wakishinda vita watavunja silaha zao zote na kutafuta zingine kama tuu pakitokea vita nyingine.

Kitendo kile kilimshangaza sana Pazi Kilama. Na alishtuka sana kuona ukoo ule ukifanya tukio hilo la ajabu sana. Na kutokana na hiyo, ndipo pazi alipoamua kusema kuwa:

"kuanzia leo hamtaitwa Wang’hoo, na jina lenu litakuwa Wabena migoha. Ambapo kwa lugha ya kizaramo kubena maana yake ni kuvunja na migoha ni mikuku".

Na alifanya hivi kwa lengo la kutunza kumbukumbu, kwani kila vita bwana Pazi alikuwa akiweka historia kwa lengo la Watu kuja kujifunza. Hivyo pazi aliamua kuwaita Wabena Migoha. Na kutokana na mahusiano mazuri Wabena walipata kuishi na kushirikiana na Wazaramo, walizaliana na kuongezeka na walitawanyika sehemu mbalimbali kutokana na shughuli zao.

Na mpaka Wazungu wanafika katika ardhi ya Tanzania kwenye miaka ya 1850, walikuta kabila linalojitosheleza na likiwa na watu wake wengi sana.. Na kutokana na mabadiliko ya waandishi wa kikoloni walijaribu kufupisha jina lile, yani kutoka Wabena Migoha na kuja kuwa Wabena.

Hii ndiyo asili ya jina Wabena. Bado historia hii ni ndogo sana hivyo ni wakati wa kila mtanzania kuikuza historia ya kabila hili.