HISTORIA YA WASUKUMA


HISTORIA YA WASUKUMA
___________________

Wasukuma ni kabila kubwa
zaidi likipatikana nchini Tanzania, linakadiriwa kufikia watu milioni 5.5 idadi inayewakilisha asilimia 16 ya wakazi wa nchi kwa ujumla.Wasukuma ina maana ya watu waupande wa kaskazini, lakini maana hii haiwakilishi maana halisi ambayo watu wengi huitafsiri kwa mfano wasukuma hutumia alama ya utambulisho (dira) kwa eneo fulani kwa viashirio vya makabila, kwa mfano wa jina kama hili Kiya hili lina maana ya Mashariki ambako ni mawio ya jua, huu ni utambulisho ambao haukufananishwa ama kuitwa kwa jina la kabila fulani, mfano mwingine ni upande wa Dakama ambapo yatambulisha kama eneo la unyamwezini lakini zaidi ya mpanuko wake ni upande wa kusini

zaidi ya hapo neno hili hutumiwa sana na kabila la wanyamwezi ili kutambulisha eneo la wasukuma ambapo wasukuma nao husema ‘’’dakama’’’,

upande mwingine ambao unapewa alama ya utambulisho ni UShashi maana yake ni upande wa kabila ya washashi na neno hili washashi ni mkusanyiko wa makabila ya mkoa wa mara japo pia neno hili shahi linamaanisha kabila la wakurya ambalo pia mpanuko wake unakomea hapo,

ambapo zaidi ya hapo eneo zima la upande huo unamaanisha upande wa kaskazini na upande wa mwisho kutambulishwa ni Ngw’eli, neno hili halikupewa kabila na badala yake linawakilisha upande wa magharibi (dira), ambako ni machweo ya jua. " Wasukuma wenyewe hulirejea jina hili kama Basuguma kwa (wingi) na Nsuguma kwa (umoja).

Wasukuma huishi eneo la kaskazini magharibi mwa Tanzania karibu na mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria, na maeneo mbalimbali ya utawala ya wilaya ya Nyamagana, mkoa wa Mwanza, upo pia kusini magharibi mwa mkoa wa Mara, w:Mkoa wa Simiyu na Mkoa wa Shinyanga. Eneo la kaskazini la makazi yao ni katika maarufu Plain w:Serengeti. Familia za wasukuma wengi sana wamehamia maeneo ya kusini kuelekea maeneo ya mkoa wa Rukwa ambao baadae umegawanyw’a na kuzaa mkoa wa Katavi, wakipita maeneo ya kabila ya Wapimbwe. Na hivyo kufanya makazi katika eneo hili la kijiji cha Wapimbwe.

Eneo hili la wasukumaland ambalo linakadiriwa kuwa na ukubwa wa mita za mraba 910 hadi 1200 sawa na futi Kigezo:Kubadili:. Mwinuko wake unakadiriwa kuwa inchi Ishirini hadi arobaini (Kigezo:Convert/wa) ya ujazo wa mvua kutoka Novemba hadi mwezi Machi. Kiwango cha juu cha joto hutegemea angalau ni kutoka Kigezo:Convert/ya wakati kiwango cha chini nyakati za usiku hushuka na kufikia 15 °C (59 °F). Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi na hivyo pia kuongezeka kwa wakulima wa mbogamboga.

Shughuli za kiuchumi.
******

Shughuli kuu za kiuchumi kwa wasukuma ni kilimo,uvuvi, ufugaji na biashara. Pamba ndio zao kuu la kibiashara kwa wasukuma, ambao pia hulima mazao mengine kama mpunga, tumbaku, mahindi,Viazi,Dengu na matunda(Kisiwani ukerewe) Wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvuvi, madini mbalimbali kama vile dhahabu, almasi na madini mengineyo huchimbwa katika maeneo mbali mbali mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

Wasukuma pia wanajihusisha sana sana na kilimo cha mazao ya nafaka na mifugo ya aina mbali mbali. Maeneo ya Shinyanga wanalima mazao ya nafaka kama Mahindi na Mpunga.

Maeneo yaliyo na madini:
******

Wasukuma wamezungukwa na madini mbalimbali. Yafuatayo ni maeneo yaliyo na madini.

1.Mwadui (Huku kuna madini ya almasi ambayo kwa kiwango kikubwa huipatia serikali pesa za kigeni) 2. Maganzo (Vilevile eneo hili limewekwa kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo wa almasi, eneo hili liko magharibi ya Mwadui.)