HISTORIA YA WAZARAMO

HISTORIA YA WAZARAMO




HISTORIA FUPI YA WAZARAMO
_________________________

Wazaramo (1906)
Wazaramo ni kabila kutoka eneo baina ya Dar es Salaam na Bagamoyo, nchini Tanzania. Mwaka 2000 idadi ya Wazaramo ilikadiriwa kuwa 656,730. Lugha yao ni Kizaramo.

Wazaramo ni sehemu ya Wabantu. Mababu wanaaminika waliingia katika eneo la Tanzania katika milenia ya kwanza. Historia yao ya kimdomo inasema ya kwamba walihamia pwani katika mazingira ya Daressalaam kutoka Uluguru (Morogoro) katika karne ya 18.

Walipokaa kwenye pwani walikuwa karibu na makazi ya Waswahili wakaanza kufaamiana na Uislamu. Taarifa za wakoloni Wajeruami mwanzoni wa karne ya 20 zinaonyesha ya kwamba wakati ule Uislamu ulikuwa umeenea kati ya Wazaramo na waliendelea kujiunga nayo haraka. Siku hizi idadi kubwa wa Wazaramo ni Waislamu.

Jiji la Dar es Salaam lilikua haraka na kumeza vijiji vingi vya Wazaramo na wengine walihamia jijini wakitafuta kazi.

Mila na desturi

Taarifa za mwanzo wa karne ya 20 zasema ya kuwa Wazaramo walikuwa na desturi za pekee tofauti na wakazi wengine ya pwani.

nyumba zao zilikuwa kubwa na za umbo la mraba.
mazishi yalikuwa ya kulaza maiti makaburini mwanaume akilazwa upande wa kulia na mwanamke akilazwa upande wa kushoto; kichwa kuelekea magharibi.
Kaburi ilipambwa kwa kusimamisha ubao mguuni na sanamu ya ubao mwenye kofia upande wa kichwa; kaburi lote lilifunikwa kwa paa ya manyasi
mabinti walipewa "mwana wa kiti" (mwanasesere wa kike wa ubao) waliotumia kuanzia kubalehe hadi kumzaa mtoto wa kwanza

Post a Comment

0 Comments