Bara la Afrika ni moja la bara ambalo lina historia ndefu sana. Historia ambayo iljengwa na Waafrika wenyewe na zingine zilijengwa na watu ambao sio waafrika lakini wakishirikiana na Waafrika .Kwa upande mwingine kuna tamaduni ambazo zilianzishwa na waafrika wenyewe ili kukabiri mazingira yao na zipo tamaduni zingine ambazo Waafrika walizianzisha kutokana na ujio wa wageni.
Miongoni mwa makabila ambayo tamaduni zao zimletwa kutokana na ujio wa wageni mfano mzuri ni Wamakonde kutoka kusini mwa Tanzania na Wasara au Wakeeni kutoka kusini mwa nchi ya Chad. Makala hii fupi tutaangalia kabila la Wasara na utamaduni wao wa kujichora usoni na kutoboa midomo wenye kuhusiana na baishara ya utumwa.Lakini ukweli ni kwamba kabila hili halikuandika chochote juu ya historia yao, hivyo ilikuwa kazi kwa wanakiolojia kufanya utafiti. Wanaakiolojia walifanikiwa kuvumbua vitu vingi vilivyosaidia kufahamu historia ya kabila la Wasara. Kwa mfano, mabaki ya nyumba, michoro, vyungu, vifaa vya chuma, mawe na vyombo mbalimbali ambavyo vilifanyiwa utafiti wa akiolojia.
Wasara au wakareeni ni moja ya kabila linalopatikana katika familia lugha ya Nilo-Saharani. Lugha wanayoongea inaitwa Bongo-Bagirmi .Wanapatikana kusini mwa nchi ya Chad na wachache wanapatikana katika nchi ya Afrika ya kati. Ni miongoni mwa makabila ambayo tamaduni zao zinauhusiano mkubwa na biashara ya utumwa ilikuwa ikihusisha kuvuka jangwa la Sahara. Wasara ni miongoni mwa makabila ambayo kwa sasa tamadunin zao zinapotea kutokana na tamaduni hizo kuhusishwa na masuala ya utumwa.
Yaani kama vile historia ya kujichonga meno, kuchanja chale na kutoboa Ndonya kwa kabila la wamakonde wanaopatikana kusini mwa Tanzania.Kabila hili la Wasara lina mganyiko ambao unatokana na utofauti wa kijiografia, kisiasa na wakati mwingine hata kiukoo. Asili ya neno Sara linausiana sana na Watu wa Misri juu y a uwepo wa Mungu Jua. Neno hili ni la kiarabu lenye maana ya watoto wa Ra, Ra alikuwa mungu jua wa watu wa Misri.
Asili ya jamii hii ya Wasara ilianzia huko Afrika ya kaskazini katika maeneo yalifahamika kama mto Chari na ziwa Chad. Wakazi wa mwanzo wa jamii hizi walifahamika kama Wasao ambao waliishi maeneo hayo takribani karne ya 6 kabla ya kristo kuzaliwa. Kwenye miaka ya 900-1000 miji ya wakazi ya Wasao ilikuwa imeendelea kwa kiasi kikubwa.Kama ilivyokuwa kwa Wabantu, pia Wasao waliweza kuhama kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na uvamizi wa Waarabu. Hivyo wakagawanyika wapo waliobaki hapo na wengine walienda Kaskazini mashariki mwa mto Nile.Kutokana na kuhama huko nchi ya
wakazi wa Wasao ikaanguka na ndio ukawa mwisho wa jamii za Waso na kukawa na jamii ya Wasara mara baada ya kuchangamana na Watu wa Misri.
Kwenye karne ya 9 na ya 10 biashara ya utumwa ilikuwa imeshamiri kaskazini mwa bara la Afrika. Miongoni mwa makabila yaliyoathiliwa sana kiutamaduni ni Wasara. Utamaduni wa kujichora usoni na kutoboa midomo kabla ya utumwa haukuwepo, ila tamaduni hizi zilikuja kuwepo mara baada ya biashara ya utumwa kushamiri. Kwa kawaida hakuna mtumwa aliyependa kuwa mtumwa, bali watu walikuwa wakilazimishwa kuwa watumwa.Hivyo kwa jamii za Waafrika suala la utumwa lilipingwa sana.Baishara ya utumwa ilihitaji watu waliokamilika kimaumbile na kimuonekano, yaani mtumwa hakupaswa kuwa na jeraha wala michubuko.
Hivyo jamii za Wasara waliamua kujichora usoni na kutoboa midomo kwa kutumia kisu cha moto kwa ajili ya kujiweka alama, ili waarabu wakija wasiwachukue utumwani, kwani alama hizo zilikuwa kama vidonda. Hivyo kila mwanajamii alipaswa kufanya hivyo, kwani asipofanya hivyo atachukuliwa utumwa. Hivyo ikawa hivyo vizazi hadi vizazi na ikarithisha kama sehemu ya utamaduni. Na kwa wakati huo asijichora aliitwa mtumwa na alitengwa na jamii(historia hii inafanana na ile ya wamakonde). Ukweli ni kwamba uchorwaji wa michoro hiyo usoni na utoboaji wa midomo ilikuwa na maumivu makubwa sana, ilichukua wiki 2 hadi 3 kwa mtu kupona maumivu hayo.Kwa sasa utamaduni huu unaonekana kupitwa na wakati.
Mfumo wa ndoa wa jamii ya Wasara upo tofauti kidogo na jamii zingine za kiafrika. Kulingana na mila na desturi za wasara, mume anapaswa kutoa mtama kwa familia ya mke ili apate kuoa. Ndoa za mitaala zilikuwepo. Na kwa upande mwingine taraka zilihusikla kwa kiasi kikubwa.
Dini na imani kwa jamii za Wasara ilikuwa kama ifuatavyo, kipindi kabla ya ujio wa waislamu wasara walaiabudu miungu yao ya Jua. Na mara kipindi cha waislamu wapo walikuw waislamu na wapo walioendelea kuwa na imani zao zingine. Na mwisho kipindi cha ukoloni wapo waliokuwa wakristo na wengine wakiwa waislamu na dini zingine za jadi.
0 Comments