
Wanajeshi wa Tanzania walipita maeneo mengi kuhakikisha kuwa hakuna askari wa Iddi Amin aliyebakia Uganda. Ingawa katika maeneo hayo wanajeshi wa Tanzania walipokewa vyema na raia wa Uganda, walionywa kuwa eneo la West Nile hali ilikuwa tofauti kwa sababu hiyo ilikuwa ni ngome ya Amin.Kwa mujibu wa jarida la Africa Currents, watu wa eneo hilo walifikia hata hatua ya kuweka sumu kwenye mazao yao na kuwapa askari wa Tanzania.Kitabu cha War in Uganda kinaandika kuwa katika viunga vya mji wa Masindi, askari watatu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambao walikula ndizi walizopewa na wakazi wa eneo hilo waliugua ghafla na kufariki dunia. Ilidaiwa kuwa walitia sumu hata kwenye maji ambayo walidhani Watanzania wangeyanywa.Kiasi cha askari 10,000 wa Amin walikuwa wamekimbilia eneo hilo mara baada ya Kampala kukombolewa. Mabasi, malori na magari mengi ya kawaida yaliyoibwa maeneo mengi ya Uganda yalikutwa eneo hilo la West Nile. Mengi yalikuwa yametelekezwa njiani baada ya kuharibika.Kwa majuma kadhaa, maofisa waandamizi wa Tanzania mjini Dar es Salaam na ofisi ya Jenerali David Musuguri mjini Entebbe walikuwa wakijadiliana namna ya kushughulikia tatizo la West Nile. Baadaye iliamuliwa kuwa eneo hilo litekwe kilomita moja baada ya nyingine.Wanajeshi wa Tanzania walipofika maeneo hayo walikuta hoteli za kitalii za Paraa na Chobe zikiwa zimeporwa na wanajeshi wa Amin. Hoteli hizo zilikuwa katika hifadhi ya Kabelega. Askari hao walibomoa hata baadhi ya kuta za hoteli hizo ili wapate kuiba. Hata nyaya za umeme za majengo zilitolewa.
Wanajeshi wa Tanzania walipita maeneo mengi kuhakikisha kuwa hakuna askari wa Iddi Amin aliyebakia Uganda. Ingawa katika maeneo hayo wanajeshi wa Tanzania walipokewa vyema na raia wa Uganda, walionywa kuwa eneo la West Nile hali ilikuwa tofauti kwa sababu hiyo ilikuwa ni ngome ya Amin.
Kwa mujibu wa jarida la Africa Currents, watu wa eneo hilo walifikia hata hatua ya kuweka sumu kwenye mazao yao na kuwapa askari wa Tanzania.
Kitabu cha War in Uganda kinaandika kuwa katika viunga vya mji wa Masindi, askari watatu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambao walikula ndizi walizopewa na wakazi wa eneo hilo waliugua ghafla na kufariki dunia. Ilidaiwa kuwa walitia sumu hata kwenye maji ambayo walidhani Watanzania wangeyanywa.
Kiasi cha askari 10,000 wa Amin walikuwa wamekimbilia eneo hilo mara baada ya Kampala kukombolewa. Mabasi, malori na magari mengi ya kawaida yaliyoibwa maeneo mengi ya Uganda yalikutwa eneo hilo la West Nile. Mengi yalikuwa yametelekezwa njiani baada ya kuharibika.
Kwa majuma kadhaa, maofisa waandamizi wa Tanzania mjini Dar es Salaam na ofisi ya Jenerali David Musuguri mjini Entebbe walikuwa wakijadiliana namna ya kushughulikia tatizo la West Nile. Baadaye iliamuliwa kuwa eneo hilo litekwe kilomita moja baada ya nyingine.
Wanajeshi wa Tanzania walipofika maeneo hayo walikuta hoteli za kitalii za Paraa na Chobe zikiwa zimeporwa na wanajeshi wa Amin. Hoteli hizo zilikuwa katika hifadhi ya Kabelega. Askari hao walibomoa hata baadhi ya kuta za hoteli hizo ili wapate kuiba. Hata nyaya za umeme za majengo zilitolewa.
Maelfu ya askari wa Tanzania walisogezwa eneo hilo tayari kushambulia.Siku moja kabla ya kushambulia, eneo hilo lilichunguzwa kwa uangalifu. Hata hivyo, wapiganaji na maofisa waandamizi hawakuona kama kulikuwa na watu ng’ambo ya pili ya Mto Pakwach kuelekea West Nile.Baada ya kujiridhisha, askari wa Tanzania waliamua kuvuka mto kuelekea West Nile. Daraja la Pakwach halikuwa na ulinzi wowote wa askari a Amin kama ilivyodhaniwa.Baadaye JWTZ ikaona hakukuwa na sehemu nyingine yoyote ya Uganda ambayo ilihitaji uangalifu wa kijeshi kuliko maeneo yale ambayo tayari walikuwa wamepita. Ikiwa askari wa Amin walikuwa wamepanga kupigana, basi wangefanya hivyo kwenye Daraja la Pakwach.Askari wa Tanzania walipofika eneo la Nebbi, walishangaa wakilakiwa kwa shangwe. Wakazi wengi waliwapa chakula na vinywaji, lakini askari hao walishaonywa wasile wala kunywa chochote wanachopewa huko.Mapokezi hayo yalikuwa ni faraja kwa askari wa Tanzania na yaliendelea kuwa hivyo kijiji baada ya kijiji kuelekea Arua. Kote huko hakukuwa na dalili yoyote ya kuwapo kwa askari wa Amin isipokuwa risasi chache zilizosikika wakati wakivuka Mto Ora.Lakini kuelekea Arua hakukuwa na dalili zozote za askari wa Amin. Arua ulikuwa mji wa mwisho wa Uganda kukombolewa na hapo ndipo ilipomalizikia vita iliyodumu kwa miezi minane.Kulikuwa na taarifa zilizodai kuwa Amin alikuwa amejificha Arua. Zile sababu za awali za kujizuia kumuua Amin zilikuwa zimeshatoweka na sasa askari wa Tanzania walikuwa wanawaza jambo ambalo wengemfanya ikiwa watamtia mikononi mwao.Kitabu cha War in Uganda kinasema kulikuwa na amri kuwa ikiwa Amin angepatikana akamatwe badala ya kuuawa. Maofisa wa Serikali mpya ya Uganda waliwaambia askari wa Tanzania kwamba walitaka Amin akamatwe ili ashtakiwe.Brigedia Roland Makunda alikabidhiwa kazi ya kuitwaa Arua na kazi ya kuidhibiti njia ya kutoka Arua alikabidhiwa Brigedia Hemedi Kitete.Katika kambi ya Bondo, kulitokea mapambano kidogo na askari wa Amin. Mashambulizi ya askari wa Amim yalikuwa ya mfululizo. Askari wa Tanzania walipojibu mapigo, milio ya risasi na mabomu ilisikika kama vile vita vimeanza upya.Giza lilikuwa limeshaingia wakati magari ya wagonjwa yalipofika kuwabeba majeruhi. Askari sita wa Tanzania waliuawa katika tukio hilo na wengine 14 kujeruhiwa. Hakuna askari wa Amin aliyeuawa.Asubuhi viunga vya mji wa Arua vikawa vimeshatekwa na Brigedi ya 206.Brigedia Makunda akapata habari kuwa askari wa Amin walikuwa wamejichimbia katika Hoteli ya Rhino na kwamba raia wote walikuwa wameshakimbia. Alitaka kuilipua hoteli hiyo usiku huo.Huo ndio ungekuwa mwisho wa vita kwa Brigedi ya 206 kwa sababu Brigedi ya Minziro ilikuwa inaondoka Arua kuelekea kwenye mpaka wa Uganda na Sudani.Usiku askari wa Tanzania walishambulia kwa mabomu na kulipopambazuka Brigedi ya 206 ikaingia katika mji wa Arua. Hakukuwa na dalili zozote za kuwapo kwa Amin katika eneo hilo.Mali za nyumba yake aliyoimiliki Arua zilikuwa zimeporwa sawasawa na zilivyoporwa za nyumba nyingine.Nje ya nyumba hiyo liliegeshwa gari lake la kifahari aina ya Maserati. Askari wa Tanzania walijaribu kuliwasha lakini halikuwaka, wakaamua kuliacha.Eneo hilo walikamatwa waliokuwa mawaziri wa Amin ambao ni Waziri wa Elimu, Brigedia Barnabas Kili; Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Luteni Kanali Michael Ambia na Ofisa Utawala na Mafunzo jeshini, Meja Vincent Yekoko. Watatu hao waliamua kuendelea kuwasubiri wanajeshi wa Tanzania mjini Arua badala ya kukimbilia Sudani au Zaire (DRC) pamoja na askari wengine wa Amin.Mawaziri hao wa Amin walipohojiwa ndipo walipotoa siri kuwa Amin alikuwa ameshaikimbia Uganda. Alikwenda Arua mara baada ya Kampala kukombolewa na muda mfupi baadaye akaondolewa Uganda kwa ndege ya Libya na alipoondoka aliliacha jeshi lake bila uongozi na likageuka kuwa kundi la uporaji na mauaji.
Maelfu ya askari wa Tanzania walisogezwa eneo hilo tayari kushambulia.
Siku moja kabla ya kushambulia, eneo hilo lilichunguzwa kwa uangalifu. Hata hivyo, wapiganaji na maofisa waandamizi hawakuona kama kulikuwa na watu ng’ambo ya pili ya Mto Pakwach kuelekea West Nile.
Baada ya kujiridhisha, askari wa Tanzania waliamua kuvuka mto kuelekea West Nile. Daraja la Pakwach halikuwa na ulinzi wowote wa askari a Amin kama ilivyodhaniwa.
Baadaye JWTZ ikaona hakukuwa na sehemu nyingine yoyote ya Uganda ambayo ilihitaji uangalifu wa kijeshi kuliko maeneo yale ambayo tayari walikuwa wamepita. Ikiwa askari wa Amin walikuwa wamepanga kupigana, basi wangefanya hivyo kwenye Daraja la Pakwach.
Askari wa Tanzania walipofika eneo la Nebbi, walishangaa wakilakiwa kwa shangwe. Wakazi wengi waliwapa chakula na vinywaji, lakini askari hao walishaonywa wasile wala kunywa chochote wanachopewa huko.
Mapokezi hayo yalikuwa ni faraja kwa askari wa Tanzania na yaliendelea kuwa hivyo kijiji baada ya kijiji kuelekea Arua. Kote huko hakukuwa na dalili yoyote ya kuwapo kwa askari wa Amin isipokuwa risasi chache zilizosikika wakati wakivuka Mto Ora.
Lakini kuelekea Arua hakukuwa na dalili zozote za askari wa Amin. Arua ulikuwa mji wa mwisho wa Uganda kukombolewa na hapo ndipo ilipomalizikia vita iliyodumu kwa miezi minane.
Kulikuwa na taarifa zilizodai kuwa Amin alikuwa amejificha Arua. Zile sababu za awali za kujizuia kumuua Amin zilikuwa zimeshatoweka na sasa askari wa Tanzania walikuwa wanawaza jambo ambalo wengemfanya ikiwa watamtia mikononi mwao.
Kitabu cha War in Uganda kinasema kulikuwa na amri kuwa ikiwa Amin angepatikana akamatwe badala ya kuuawa. Maofisa wa Serikali mpya ya Uganda waliwaambia askari wa Tanzania kwamba walitaka Amin akamatwe ili ashtakiwe.
Brigedia Roland Makunda alikabidhiwa kazi ya kuitwaa Arua na kazi ya kuidhibiti njia ya kutoka Arua alikabidhiwa Brigedia Hemedi Kitete.
Katika kambi ya Bondo, kulitokea mapambano kidogo na askari wa Amin. Mashambulizi ya askari wa Amim yalikuwa ya mfululizo. Askari wa Tanzania walipojibu mapigo, milio ya risasi na mabomu ilisikika kama vile vita vimeanza upya.
Giza lilikuwa limeshaingia wakati magari ya wagonjwa yalipofika kuwabeba majeruhi. Askari sita wa Tanzania waliuawa katika tukio hilo na wengine 14 kujeruhiwa. Hakuna askari wa Amin aliyeuawa.
Asubuhi viunga vya mji wa Arua vikawa vimeshatekwa na Brigedi ya 206.
Brigedia Makunda akapata habari kuwa askari wa Amin walikuwa wamejichimbia katika Hoteli ya Rhino na kwamba raia wote walikuwa wameshakimbia. Alitaka kuilipua hoteli hiyo usiku huo.
Huo ndio ungekuwa mwisho wa vita kwa Brigedi ya 206 kwa sababu Brigedi ya Minziro ilikuwa inaondoka Arua kuelekea kwenye mpaka wa Uganda na Sudani.
Usiku askari wa Tanzania walishambulia kwa mabomu na kulipopambazuka Brigedi ya 206 ikaingia katika mji wa Arua. Hakukuwa na dalili zozote za kuwapo kwa Amin katika eneo hilo.
Mali za nyumba yake aliyoimiliki Arua zilikuwa zimeporwa sawasawa na zilivyoporwa za nyumba nyingine.
Nje ya nyumba hiyo liliegeshwa gari lake la kifahari aina ya Maserati. Askari wa Tanzania walijaribu kuliwasha lakini halikuwaka, wakaamua kuliacha.
Eneo hilo walikamatwa waliokuwa mawaziri wa Amin ambao ni Waziri wa Elimu, Brigedia Barnabas Kili; Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Luteni Kanali Michael Ambia na Ofisa Utawala na Mafunzo jeshini, Meja Vincent Yekoko. Watatu hao waliamua kuendelea kuwasubiri wanajeshi wa Tanzania mjini Arua badala ya kukimbilia Sudani au Zaire (DRC) pamoja na askari wengine wa Amin.
Mawaziri hao wa Amin walipohojiwa ndipo walipotoa siri kuwa Amin alikuwa ameshaikimbia Uganda. Alikwenda Arua mara baada ya Kampala kukombolewa na muda mfupi baadaye akaondolewa Uganda kwa ndege ya Libya na alipoondoka aliliacha jeshi lake bila uongozi na likageuka kuwa kundi la uporaji na mauaji.
VITA YA KAGERA: Vita yamalizika, JWTZ waendelea kutamba Uganda

Kutekwa kwa mji wa Arua kukawa ndio mwisho wa Vita vya Kagera. Vita iliyoanza rasmi Oktoba 1978 kwa majeshi ya Iddi Amin kuvamia na kuteka eneo la kaskazini mwa Mto Kagera ikamalizika kwa majeshi ya Tanzania kuteka miji mingi ya Uganda na hatimaye kumaliza kwa kuuteka mji wa Arua.
Askari wa Iddi Amin waliofanikiwa kuyatoroka majeshi ya Tanzania walikimbilia Zaire na Sudan huku wakiapa kuwa wanakwenda kujipanga ili waje kuishambulia Serikali mpya ya Uganda.
Siku moja baada ya mji wa Arua kukombolewa, askari wa Tanzania walikutana na vijana wawili wakikimbia kuelekea kusini wakitokea upande wa Sudan.
Walipohojiwa walisema walitekwa kusini mwa Kampala na askari wa Amin waliokuwa wakikimbia kuelekea kaskazini mwa mji huo na kwamba, walipelekwa kusini mwa Sudan bila hiari yao pamoja na vijana wengine ambako waliambiwa wangepewa mafunzo ya kijeshi na siku moja wangerejea Uganda.
Kwa mujibu wa kitabu cha Kuzama kwa Idi Amin cha Baldwin Mzirai walipokuwa wakipelekwa Sudan, “vijana hao pamoja na wengine wawili, waliruka kutoka kwenye lori la kijeshi lililokuwa likiwasafirisha, wakakimbilia msituni...”
Kitabu cha War in Uganda kinasema vijana hao walisimulia kuwa wao pamoja na wengine watatu walifanikiwa kuruka kutoka kwenye lori kabla halijafika kwenye mpaka wa Uganda na Sudan na kwamba wenzao watatu walioruka pamoja, wao walionekana na waliuawa kwa kupigwa risasi walipokuwa wakijaribu kutoroka.
Vijana hao waliwaambia askari wa Tanzania kuwa kulikuwa na maelfu ya vijana wengine katika kambi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Luteni Kanali Yakobo Abiringa ambaye alikuwa maarufu kwa jina la ‘999’. Walisema walipewa shilingi 600 za Uganda. Na kama ushahidi, waliwaonyesha wanajeshi hao fedha hizo.
Askari wa Brigedi ya Minziro walijisikia fahari sana kuhitimisha Vita vya Kagera baada ya kuuteka mji wa Arua. Brigedia Ahmed Kitete alifika hadi Koboko, kijijini alikozaliwa Iddi Amin, kiasi cha kilomita 40 kaskazini mwa mji wa Arua.
Hata hivyo alikuta kijiji hicho kilikuwa kimeshakimbiwa na watu na hivyo hakukuwa na dalili yoyote ya kuwapo kwa askari wa Amin. Baadaye ilijulikana kuwa wakazi wa kijiji hicho walikuwa wamekimbilia Zaire ambayo mpaka wake uko umbali wa chini ya kilomita moja.
Ingawa awali Watanzania waliambiwa kuwa katika kijiji cha Koboko, nyumbani kwa Amin, Iddi Amin alikuwa amejenga nyumba ya kifahari, Brigedia Kitete na askari wake hawakuiona nyumba hiyo. Walichokuta ni nyumba ya kawaida tu ya Amin ambayo nayo, kama zilivyokuwa zile nyingine ilikuwa imeporwa kila kitu.
Gazeti la New York Times la Jumatatu ya Juni 4, 1979 liliripoti kuwa katika kijiji cha Koboko, “Watanzania walikuta tu mbwa mmoja na kuku mmoja na hakukuwa na dalili nyingine yoyote ya uhai. Wanavijiji 1,000 au zaidi walikuwa wameshakimbia ... nyumba ya Amin ilikuwa imeporwa.”
Jenerali Silas Mayunga aliungana na Brigedi ya Minziro kukamilisha siku za mwisho za vita. Walivinjari kuanzia Koboko na kupita mpaka wa Uganda na Zaire hadi mpaka wa Uganda na Sudan. Upande wa Uganda watu walikuwa wamekimbia na kuvuka mpaka.
Kila baada ya kilomita chache Jenerali Mayunga na Brigedia Kitete walikuwa wakisimamisha msafara wa askari wao na kusoma ramani. Walikuwa wakifanya hivyo kuwa na uhakika kuwa hawavuki mpaka wa Uganda na kuingia nchi nyingine kama Zaire au Sudan.
Kabla msafara huo haujafika mpakani mwa Uganda na Sudan, Mayunga aliamuru vifaru na mabasi kusimama. Askari waliteremka kutoka kwenye vyombo hivyo na kutembea kwa miguu hadi mpakani. Eneo lote hilo lilikuwa limekimbiwa.
Umbali wa mita 300 kuvuka daraja dogo ndipo ulipo mpaka wa Sudan na Uganda. Umbali wa mita nyingine 300 ndani ya Sudan walionekana wanajeshi wa Sudan wakiwa na silaha zao zikiwa zimeelekezwa kwa askari wa Tanzania. Nyuma ya wanajeshi wa Sudan kulikuwa na maelfu ya raia ambao walidhaniwa kuwa ni Waganda, pamoja na magari kadhaa yaliyokuwa na namba za usajili za Uganda.
Watanzania walijisikia vibaya kidogo kuwapo eneo hilo huku wakiwa wameelekezewa silaha na askari wa Sudan. Ingawa askari wa Tanzania waliwapungia askari Sudan, Wasudani hawakupunga.
Mayunga hakuona sababu ya kuendelea kukaa eneo hilo na kuwafanya Wasudan hao kuendelea kuwa na wasiwasi juu yao. Ingawa walitaka kupiga picha mpakani mwa Uganda na Sudan, waliamua wasifanye hivyo.
Hadi muda huo Iddi Amin hakujulikana alikokuwa. Katika makala ya gazeti la The Monitor la Uganda toleo la Jumapili ya Mei 8, 2016 chini ya makala How Amin escaped from Kampala, askari wa Amin waliokutana naye siku za mwisho za utawala wake—Luteni Kanali Galla na Staff Sajini Taban Alai—walikaririwa na gazeti hilo wakikumbuka maneno waliyoambiwa na Iddi Amin.
Sajini Alai anakumbuka Amin akimwambia, “Bunduki uliyobeba sasa ni baba yako, ni mama yako, ni dada yako ni kila kitu kwako. Usisalimu amri kwa yoyote. Nakwenda Libya kupata silaha na msaada na nitarudi kuendelea kupambana. Kuwa hodari na ilinde Arua hadi nitakaporudi.”
Ni kweli kwamba Iddi Amin alikwenda Libya kama alivyoahidi, lakini hakurudi kama alivyoahidi.
Wakiwa mpakani mwa Uganda na Sudan, Jenerali Mayunga aliwaita askari wake, akatoa hotuba fupi akiwaambia: “Mmemfundisha Iddi Amin somo ambalo hatalisahau kamwe.” Kisha akawaamuru kurejea Koboko.
Askari wa Tanzania walikumbatiana. Vifaru na mabasi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vikageuka na kuondoka mpakani. Hadi kufikia Jumapili ya Juni 3, 1979, askari wa Tanzania walikuwa wametembea umbali wa kilomita 12,000.
Itaendelea
0 Comments