KUZUILIWA KWA PATRICK OTTIENO LUMUMBA NCHINI ZAMBIA ILIKUWA NI AMRI KUU KUTOKA SERIKALI YA CHINA KUPITIA UBALOZI WAKE NCHINI ZAMBIA.PATRICK OTTIENO LUMUMBA



Ni mmoja kati ya mwanasheria machachari maarufu na mkongwe nchini Kenya (Kenyan Prominent Lawyer) ambaye pia alikuwepo  kwenye jopo la wanasheria wakuu (Kenyan Electral Commission)  ambao walitengua uchaguzi mkuu nchini humo. Ambao ulikuwa na ukakasi pamoja na udanganyifu mwingi ndani yake mwishoni mwa 2017.Amekuwa ni mtu muhimu katika maendeleo ya Afrika kwa kuibua hoja nzito ambayo imeonekana kufanyiwa kazi katika mataifa mbalimbali kwa lengo la kukafanikisha agenda 2063.

kama tunavyojua kwamba Bara la Afrika liko nyuma kimaendeleo kwa sababu ya rushwa PLO ni mwasisi na mkurugenzi  wa Ant-Corruption Movement aliyoanzisha mwenyewe mwaka 2010 ambayo pia haikudumu sana. Amekuwa mhamasishaji, mkosoaji na mshauri mkubwa kwa vijana wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na kwa viongozi walioko madarakani. Hakika ni mtu wa kipekee sana (Gifted/Talented/Oratory and Motivational Speaker). Amekuwa akiwaasa vijana na viongozi kote barani Afrika namna gani wanaweza  kujikomboa kifikra na namna ya kulikomboa bara la Afrika ambalo lipo mguu nje mguu ndani  kwa kipitindi cha miaka 60 sasa.

Prof Patrick Otieno Lumumba ni mmoja kati  ya Pan-Africanist wa kweli na mwanamageuzi ama mwanabadiliko wa uhakika ambaye kwa namna moja au nyingine Afrika na vitongoji vyake inapaswa kujivunia (The Optmist & Academician). Prof Lumumba ni moja ya watu makani na mzalendo ambae anapambana fika kuona kwamba miaka 20 baadae Bara la Afrika litakuwa la mfano na kwa asilimia kubwa liweze kujitegemea angalau kwa asilimia 80% kuweza kuhudumia watu wake na kuwafanya wafurahi kuishi Afrika tofauti na ilivyo sasa kwamba kila kona ya Afrika kunavuja damu na vilio visivyoisha. Wengi wanapenda kumfananisha na Baba wa Taifa la Congo Patrick Lumumba na wengine wanamfananisha na Dr. Osagyevo Nkwame Nkuruma Baba wa Taifa la Ghana kulingana na uwezo wake mkubwa wa kuichambua Afrika na vitongozi vyake kwa mapana Zaidi.

Ni moja kati ya wasomi wachache ambao kwa ujumla Afrika Nzima inajivunia kuwa naye ambaye anaonekana kuwafuta machozi na kuwatia moyo wanyonge kwamba bado tunayo nafasi ya kufanya vyema zaidi. Mwanasheria huyu amekuwa mtetezi mkubwa wa wanyonge kwa kupigania utawala bora na Sheria (Rule of Law),  uwajibikaji na uwazi  kote barani Afrika na kupinga vikali nchi kuongozwa kwa faida ya wachache yaani (Rule of Mob & Kleptocracy). 

Amekuwa mstari wa mbele kutokufumbia macho maovu na uvunjifu wa Amani unaoendelea Afrika. Amekuwa akikosoa vikali Serikali ambazo haziwajibiki ipasavyo kama vile Congo, Zimbabwe, Cameroon, Burundi, Togo, Nigeria, Sudan pamoja na Afrika ya kati na mataifa mengine ambayo yanaongozwa kama gari bovu,ana maono mapana juu ya Afrika na vitongoji vyake. Lakini pia ni mshauri mkubwa dhidi ya uongozi mbaya na amekuwa akipinga waziwazi  ruswa na matamuzi mabaya ya malighafi za Serikali Kote barani Afrika (Ant-Corruption Crusader) .

PLO Lumumba ni kama vijana wengine wa kiafrika ambapo tulio wengi tunatoka katika familia za kimasikini yaana kwangu pakavu tia maji kama waswahili ama wahenga wanavyo dadavua. Alizaliwa na kukulia katika kijiji kinaitwa Usenge pembezoni kabisa mwa Ziwa Victoria huko Kenya. Na katika elimu yake ya awali yaani ya Msingi (Elimentary School) aliipatia hapo hapo kijijini kwao kilichofahamika kama Usenge. 

Patrick Loch Otieno Lumumba hakuishia hapo alihamia katika shule inaitwa St Patrick iliyopatikana Nairobi na baadae kupata elimu yake ya sekondari katika shule iliyojulikana kama Pwani Secondary School (Ordinaly Level). Kwa kuwa alionekana kupenda kusoma na kuwa mdadisi tangu utotoni mwake wala hakuishia hapo tu mnamo mwaka 1979 alijiunga na kidato cha sita (Advanced Level) katika shule iliyojulikana kama Ambira High School iliyomfungulia njia ya yeye kwenda kujiunga na chuo kikuu huko huko Nairobi miaka hiyo hiyo 80s.

Patrick Loch Otieno Lumumba alitabiliwa tangu akiwa mdogo kwamba atakuja kuwa mtu muhimu katika taifa lake na Afrika kwa ujumla maana alianza kuonyesha utashi na ufuatiliaji wa mambo na vijambo tangu akiwa mdogo alipenda sana kusoma na kufuatilia mambo ya kihistoria hususani barani Afrika. Alianza kufuata nyayo za kina Nkwame Nkurumah na Patrick Lumumba tangu akiwa kijana hivyo walimu wake  kumtabiria makubwa mbeleni. 

Patrick Loch Lumumba alipata Degree yake ya kwanza akiwa kijana mdogo sana katika miaka 23. Hakuishia hapo tu kielimu aliendelea mbele na kuchukua Shahada ya sheria (Degree of Laws) na baadae kidogo akachukua  Masters ya Sheria huko Nairobi University . Hakuishia hapo akaenda kusoma Ubelgiji katika chuo kikuu cha Ghent (University of Ghent) ambako alisomea Udaktari katika sheria (Doctor of Law), hakuishia hapo alienda kusoma Ghana (University of Cape) ambako alienda kuongeza elimu yake zaidi na kusomea kile kinachojulikana kama Doctor of Letters ambako katika mataifa mengi ya kiafrika wanaitambua kama PhD.

Kuna ambao wanamfananisha na Thoma Isodore Sankara kulingana na uweledi, utashi  na uwelewa  mkubwa juu ya Bara hili la Afrika. Ni msomi anayethubutu na kusimama kwa kukemea uongozi mbovu na wa kizandiki pasipo kuogopa kitu chochote kile ili mradi sauti isikike na ukweli ufike. Patrick Loch Otieno Lumumba ndiyo jina lake kamili, Msomi huyu alizaliwa kama wanadamu wengine tarehe 17/06/1962, kwa lugha ya kawaida alizaliwa katika kipindi ambacho mataifa mengi ya Bara la Afrika yakiwa katika harakati za ukombozi. 

Alipewa jina la Lumumba na Baba yake mzazi ambaye alikuwa anamkubali sana Baba wa Taifa la Congo Patrick Emiery Lumumba ambaye wengi walimuona kama mkombozi wa wanyonge. Amekuwa akialikwa na kuzunguka katika mataifa mbali mbali barani Afrika katika kutoa mwongozo na kukemea uongozi wotewote ambao unakwenda kinyume na mahitaji ya wananchi. Patrick Lumumba ndiyo msomi pekee mpaka sasa ambaye ameonekana kuisoma na kulifahamu kwa karibu zaidi bara la Afrika.

Amekuwa akialikwa katika mijadala mbalimbali inayohusu Afrika hususani Rushwa, Uongozi mbaya na wa kimabavu, ukiritimba, Maendeleo ya kiviwanda na kuzungumza namna gani Afrika inaweza kujinasua kutoka katika mikono ya wazungu na kuanza na  kujitegemea. Ameenda katika mataifa mengi sana kuhubiri juu ya Umoja na mshikamano wa Bara la Afrka (Pan-Afrikanisim), amepata nafasi ya kutembelea bara la Afrika ambalo pengine maprofesa wengi hawajafanikiwa kupata hiyo nafasi. 

Kuanzia mwaka 2010 mpaka 2018 amefanikiwa kushiriki katika mijadala mikubwa mfano mwaka huu alialikwa Umoja wa Afrika (AU), mapema 9/09/2018 alikuwa Afrika Kusini katika kumbukumbu ya Ya Nelson Mandela kutimiza miaka 100 tangu kuzaliwa kwake lakini siyo mara yake ya kwanza kwenda Afrika kusinia alialikwa pia katika  kumbukumbu za kijana mdogo na mtetezi wa watu weusi bwana Abrahamu Tirro katika chuo kikuu cha Limpopo na tarehe 18/7/2018 alikuwa huko akigusia juu ya Mgogoro wa Ardhi ambao umedumu kwa muda miaka zaidi ya 70 sasa (Land Problems).

Amekuwa akienda Rwanda mara kwa mara sana sana katika kuadhimisha mauji ya kimbali ya mwaka 1994 (Rwandani Memorial Genocides) alihutubia katika taifa hilo kwa mara ya kwanza 2014 lakini pia alipata kutembelea Rwanda 14/09/2018 kujumuika katika kongamano lililojulikana kama African Religious and Leadership bado hakuishia hapo kulingana na uwezo wake mkubwa wa kuongea na kulichambua vyema Bara la Afrika alialikwa tena tarehe 18/05/2018 kuzungumzia masuala ya Ulinzi na Usalama (National Security Symposium)  mbele ya viongozi wakubwa wa Kijeshi pamoja na maafisa usalama wengine amekuwa akizunguka Afrika hii kuwaamsha waliolala na wale ambao hawapendi kuona Afrika inasonga mbele (Pesmism).

Bado hakuishia hapo  Prof Ottieno Loch Lumumba amekuwa akizidi kung'aa maana ameonekana wazi kwamba yeye ni mzalendo aliyekamilika, Viongozi wa aina mbalimbali pamoja na Wasomi wanatamani kumsikiliza maana amekuwa ni chachu ya mabadiliko na kuwafanya wale wasiopenda kufikiria waanze kufikiri. Prof Loch Ottieno Lumumba alialikwa pia katika Chuo kikuu cha Daresalaam (Tanzania) tarehe 17/06/2017 kuzungumzia kile alichokiita Magulification of Afrika ambapo aliona hatua ambazo anazitumia Magufuli zingetumika Afrika nzima. Alipata pia mwaliko kutoka chuo kikuu cha  Gambia ikumbukwe tu kwamba Gambia wana chuo kikuu kimoja tuu, akiwa Gambia alizungumzia juu ya kile alichokiita Uongozi wa Afrika pamoja ni kuzungumzia mabadiliko katika Elimu ya Afrika (African Leadership & Mis-Education of Afrika) aliongea mengi sana juu ya Bara hili la Afrika.

Ni nadra sana kuona mtu anazinguka Afrika nzima kuhubiri juu ya Utawala bora na kuepuka utawala wa kimabavu baina ya Viongozi wa Afrika, amekuwa ni mtu wa kipekee sana maana anayaibua mawazo ya waasisi wa Bara hili kama wakina Nkwame Nkuruma, George Padmore, Hazisting Kamuzu Banda, Keita Modibo, Haile Selas, Muhammad Sokou Toure, Jomo kinyatta, Abrahamu Tiro, Stiven Bantu Biko Abdel Gamal Naser, Muhammad Anwar El Sadat pamoja na Mwal Julius Kambarage Nyerere. 

Patrice Otieno Lumumba amekuwa ndiyo mtu pekee kutukumbusha kwamba wapi tumetoka na wapi tunakwenda anataka kuona Afrika inapiga hatua (Afrika Arise). Mungu amemjalia kuona matatizo na kuyaweka hadharani na kuyatolea ufumbuzi amewapa changamoto viongozi wengi waliogeuza Ikulu pango la walanguzi na sehemu ya kujitajirisha, Amekuwa akizikumbusha jumia mbalimbali kama SADC, ECOWAS, EAC, AU na COMESA kutokusahau majukumu yao bali matatizo yanapotokea wanapaswa kuchukua hatua za makusudi mapema maana Bara la Afrika ni kwa ajili ya Waafrika.

Kulingana na uwezo mkubwa na uthubutu wake wa kuyaanika hadharani matatizo ya Afrika na kuyatolea ufumbuzi amekuwa ni lulu na Chachu kwa wanasiasa Chipukuzi na wale walioko Madarakani, mnamo 6/09/2017 alipata kualikwa  Namibia katika mada iliyojulikana kama  "AFRIKA UNLEASHED HER POTENTIALS' (make Afrika Better and not Bitter ). Aliongea mengi sana na kuwakumbusha Viongozi wetu kuhakikisha wanalifanya Bara la Afrika kuwa sehemu salama na siyo sehemu chungu. 

Akiwa Namibia aliwakumbusha pia Viongozi wa Afrika kwamba wawe makini na uwepo wa China ila wahakikishe kwamba wakina mama kwa watoto pamoja na Vijana wanafurahia kuishi Afrika alienda mbali sana kuhakikisha haki inatendeka kwa kila raia.  Msumbiji na Cameroon alienda pamoja na Ghana lakini pia tarehe 10/11/2018 alialikwa Havard Univarsity na wanafunzi wenye asili ya Afrika kuzungumzia tatizo la umasikini na njaa Barani Afrika amewahi kualikwa Uganda na katika mataifa mengi ambayo sijayataja hapa juu huyo ndiyo Prof Ottieno Partrick Lumumba.