Miaka ya nyuma kidogo ambayo inafamika kama miaka ya shetani kwa Bara la Afrika maana ni kipndi ambacho waafrika walionekana siyo watu na kupoteza utu kutoka katika mikono ya Wazungu ambao waliwachukulia Waafrika kama binadamu ambao hawa jakamilika hakika (Incomplete Human).Wazungu walikuja Afrika wakafanya mambo mengi pasipokupingwa wala kuingiliwa na mtu yoyote yule maana kwa wakati huo kulingana na madai ya Wazungu ni kwamba waafrika walikuwa hawajitambui na hawajui wametoka wapi wala wana kwenda wapi hayo yalikuwa ni mawazo ya wanazuoni wa kizungu mbalimbali ambao walibahatika kukanyaga Afrika wakati huo.Ikumbukwe kwamba hoja ya msingi hapa ni juu ya Chumbuko la Liberia na kwa nini wasomi wengi wanadai Liberia haikutawaliwa na ni kitu gani kilichopelekea Liberia kutokutawaliwa.
Kutoka karne ya 15 mpaka kuendelea karne ya 19-20 ulimwengu ulishuhudia maendeleo makubwa Bara la Ulaya katika kila Sekta,Ulimwengu ulishudia kuibuka kwa mataifa makubwa yenye nguvu Dunia ikiwemo Uingereza kuanzia miaka 1650s-1750s na kuendelea kufuatiwa na Ufaransa kuanzia miaka 1790s na mataifa mengine kama Austria Hungary (Modern History); Baadae kidogo walifuata Ujerumani miaka 1870s na mataifa mengine madogo madogo ambayo pia yalifika Afrika mapema sana .kukua kwao kiuchumi,kiutawala pamoja na kijeshi ndiyo kuliwafanya Wazungu waje Afrika Mapema sana na kulitawala Bara la Afrika kwa zaidi ya miaka 500,Wazungu wa kwanza kutua Afrika walikuwa ni wapelelezi/ Watafiti,wamisionari na wafanya biashara lakini wote kwa Ujumla wao walikuwa wanafanya kazi zote kwa wakati mmoja.
Ukimsoma vizuri mwanahistoria Bwana Assah (Afro-Centric Views) Okoth katika kitabu chake cha “History of Afrika” Volume 1,kinachoengelea Historia ya Afrika kuanzia mwaka 1915 mpaka mwaka 1995 ,kuna sehemu anafanunua zaidi kwa kudai kwamba wazungu walianza kuja wengi sana kuanzi karne hiyo ya 15-19 na kuna ambao walikuja kama Wapelelezi,kuna wengine walikuja kama wafanya biashara na wengine walikuja kama watalii na baadae kuondoka.Mbali na kwamba wareno walikuwa ndo taifa masikini Barani Ulaya ila waliushangaza ulimwengu kwa kuwa wa kwanza kuzunguka na kugundua (Discoveries) maeneo mengi zaidi Dunia kuwazidi Waingereza Wafaransa na mataifa mengine. waliushangaza Zaidi ulimwengu kwa wao kuwa wa Wazungu wa kwanza kukanyaga Bara la Afrika.
kwa wakati huo kila walipokanyaga Wareno walidai kwamba wao ndiyo walikuwa wazungu wa kwanza kukanyaga Afrika ,na kila walichokuwa wanakiona walidai kwamba wao ndiyo walikuwa wazungu wa kwanza kuona,wakati huo walikusanya na kuandika kila kitu walichokuwa wanakiona na kupeleka taarifa Ulaya ndiyo ukawa mwanza kutawaliwa kwa mtu mweusi (Colonization Of Afrika).Uhusiano wa Afrika na mataifa ya Bara la Ulaya ulianza mda mrefu sana, lakini Uhusiano huu ulikuwa siyo Uhusiano mzuri sana maana mmoja mwenye nguvu alikuwa anafaidika kwa kumnyonya asiye na nguvu ,wazungu wa kwanza kuja Afrika walikuwa ni watu kutoka Ureno,wakati huo Ureno ilikisemekana kuwa taifa masikini Barani Ulaya na likiwa taifa ambalo lilikuwa na idadi ndogo ya watu lakini walikuwa na uwezo wa kuzunguka Dunia wakifanya upelelezi na biashara na mataifa mbalimbali kumbe udogo wao haukuwafanya kushindwa kuzunguka Dunia.
kipindi hicho ilikuwa ni Karne ya 15 ambapo Dhahabu na Almasi ilikuwa inatafutwa kwa machozi na Damu Barani Ulaya ,ambapo wafalme walikuwa ndiyo wahitaji wakubwa mno,maana kwa wakati huo ili uwe na nguvu na kuheshimika ulipaswa kuwa na shehena ya kutosha ya Almasi ama Dhahabu,Wareno waliwasili kwa mara ya kwanza Afrika uko Cape Verde na baadae mwaka 1470s walitua Gold Coast (Ghana) hapo walikaa kidogo na kujenga Ngome kubwa ya kibiashara iliyojulikana kama Elimina na huko walitawala biashara ya Dhahabu kati ya mataifa ya Afrika na Ulaya .Uku tukiendelea na Utangulizi huu ikumbukwe kwamba tayari waafrika katika maeneo ya Afrika Magaribi tayari walikuwa wameanza kusafirishwa kupelekwa Barani Ulaya kama watumwa japo kwa kiasi kidogo.
Huko Ghana walitwaa Dhahabu nyingi sana na kupeleka kwa Ureno miaka hiyo,wazungu wameanza kuja Afrika mda mrefu sana na wakati huo watu kutoka Afrika walikuwa hawajua thamani na matumizi ya Dhahabu ama Almasi, taarifa ziliendelea kusambaa kuhusu Afrika na utajiri wake barani kote Ulaya,na kulingana na taarifa za wapelelezi wa kireno Basi Ulaya nzima apata taarifa kwamba Afrika ndiyo sehemu pekee ambayo wanaweza wakapa mahitaji yao kwa njia raisi.Siku zilikuwa zinazidi kukatika kipindi chote hicho Wareno hao walitoka Afrika magaribi na kuambaa na ukanda wa Bahari Atlantiki na kutua Afrika kusini ,kundi hili liliongozwa na Bartolomeo Diaz huyu alikuwa mpelelezi maarufu sana wa kireno na walifika Afrika kusini na hapo walipofika wakapaita Cape of good Hope hii ilikuwa ni mwaka 1487.Ni miaka ambayo tayari wazungu walikuwa wanakuja Afrika kwa wingi mno lakini wengi kwa ajili ya Biashara na wengi wao waliishia Afrika magaribi na Afrika Kaskazini lakini wengi wao wakiwa wareno.
Wapelelezi hawa wa kireno hawakuwa peke yao hakika bali walitumwa na mpelelezi maarufu na mkongwe katika masuala ya Uvumbuzi na upelelezi (Age of Discoveries) uko Barani Ulaya,huyu ndiyo mwasisi au baba wa uvumbuzi na upelelezi katika kizazi chake,Mtaalamu uyu alijulikana kama Prince Henry The Navigator.Ni vizuri ikimbukwe kwamba jina la “Navigator” alipewa kamaa jina lake la utani ama Nick name kulingana na uwepesi wake wa kuzunguka hii Dunia na kugundua maeneo mengi sana ambayo yaliwapa wepesi wazungu wengine kuja Afrika na kwenda maeneo mengine Duniani,alikuwa mtashi na mwenye akili nyingi juu ya masuala ya upelelezi na Uvumbuzi.
The Navigator alikuwa mtoto wa nne wa Mfalme John I wa Ureno kwa wakati huo,anatambulika na anaheshimika sana kama mmoja wa watu walichangia sana katika uchumi wa Ureno miaka hiyo na ni mmoja kati ya watu wa kwanza kufanya upelelezi Duniani kote na aligundua vitu vingi na maeneo mengi yanayojulikana leo na huyu ndiyo aliyowa wafungulia njia wazungu wengine kuja Afrika na kulitawala vyema.Historia inamtambua mtaalamu huyu maana yeye ndiyo aliyewafungulia njia wakina Christopher Columbo na wengine wengine wapelelezi wengi,Kwa wakati huo alifanikiwa kugundua na kufika katika maeneo mengi sana na pamoja na kugundua njia za kuelekea katika maeneo mbalimbali,si mwingine huyu aliitwa Henry the Navigator.
Mnamo tare 01/03/1498 kundi lingine la wareno liliwasili pwani ya Bara la Afrika sana sana Malindi Sofara,Kilwa na Mombasa pia ,kundi hili liliongozwa na mtaalamu Vasco Da Gama,mtaalamu huyu wengi wanamtambua sanaa kulingana na umaarufu wake katika historia akiwa katika umri mdogo wa miaka 20s kwenda 30s alifanya mambo makubwa na ya kushangaza.Kwa wale ambao walielewa vizuri Historia ya Afrika watakuwa wanafahamu kilichikuwa kinaendelea miaka hiyo,lakini pia bwana Vasco Dagama alikuwa ndiyo Mzungu wa kwanza kufika Calicut uko India.Alifika katika maeno mengi sana na kama kiongozi wa Wareni walifanikiwa kujenga ngome nyingi sana za kireno na walifanikiwa kushika maeneo mengi ya kibiashara Afrika mashariki na Afrika magaribi pia.Hawa ndiyo watu wa mwanzo kabisa kukanyaga Bara la Afrika na walichukua taarifa nyingi mno juu ya Afrika na kupeleka Ulaya na huo ndiyo ukawa mwanzo wa Wazungu kuanza kuingia Bara la Afrika na kuanzisha kile kilichoitwa Colonialism in Afrika.
Wanaosema Afrika tulikuwa nyuma kimaendeleo basi Walidanganya hakika,yalikuwa ni mawazo ya wenzetu wazungu,mtazamo huu uliletwa na wazungu kipindi wanakuja Afrika, ambapo katika historia nadharia hii inajulikana kama Euro-Centric Views,wazungu walikuja Afrika kipindi ambacho kiukweli Bara la Afrika lilikuwa limepiga hatua katika nyanja mbalimbali,kisiasa,kijamii na kiuchumi pia bali jambo hili linapingwa sana na wazungu kwamba Afrika kulikuwa hakuna maendeleo yoyote yale.History Demostrate Time Without Numbers,Mnamo karne ya 15,Wareno wakiwa wanazunguka Dunia hii walibahatika kukanyaga Afrika kama nilivyoelezea kwenye makala juu ya chimbuko la Leberia na Sierra Leon. Katika sababu kuu iliyowafanya wareno waje Afrika kulingana na mtazamo wao ni kwamba walikuwa wamekuja kumtafuta kiongozi mmoja mkubwa wa kidini Aliyefahamika kama PRESTER JOHN kutoka Ethiopia.
Prester John Kutoka Ethiopia alikuwa ni moja wa watu maarufusa mno kaskazini mwa Afrika kwa ujumla wake,alikuwa ni mtu mwenye mguvu mno ambaye karne hiyo ya 15 taarifa zake zilifika mpaka Barani Ulaya,na moja ya Sababu ya Wareno kuja Afrika ni kumtafuta Prester John wa Ethiopiaa.Lengo la wareno kumtafuta Kiongozi huyu wa kidini Prester ni kutaka kufanya nae biashara maana walitambua kwamba kulingana na Umaarufu wake ingekuwa raisi wa kufanya nao Biashara kaskazini mwa Afrika,hivyo wakimtafuta kwa mda mrefu lakini bila mafanikio yoyote yake na historia haionyeshi popote pale kama Wareno walifanikiwa kumpata kiongozi huyo wa kidini aliyejulikana kama Prester John kutoka Ethiopia.
Kulingana na mada yenyewe kuwa ndefu kidogo ifahamike tu katika Historia kwamba siku zilienda kwa kasi sana na kwa mara ya mwisho wafanya biashara wa kireno na Wapelelezi wao waliondoka Afrika Mashariki rasmi mwaka 1700 kuelekea India lakini kwa wakati huo wote tayari Biashara ya Utumwa ama ya kuchukua waafrika kuwapeleka Ulaya na Marekani ambapo kwa wakati huo ilijukana kama NEW WORLD kulingana na Christopher Columbas,Biashara hiyo ilikuwa imeshamiri na imenoga sana.Historia inaonyesha kwamba kipindo hicho watumwa walikuwa wanahitajika zaidi kuliko dhahabu ama almasi,watumwa walisakwa kuliko kawaida na kupelekwa kufanya kazi Barani Ulaya na Maeneo mengine na hali hii ilitokea sana Afrika magaribi na Kaskazi Mwa Afrika.
Inaendelea Sehemu ya II...