NI HUKO FARM 17 NACHINGWEA MKOANI LINDI.
Kihistoria eneo la farm 17 lina mengi ya kujifunza juu ya harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika. yaani kwa nchi kama Msumbiji na Afrika ya Kusini.
Huu msitu maarufu kwa jina la "MSITU WA SOKOINE" ulikuwa mmoja wa Msitu ambao wanajeshi na wanaharakati wa Kupigania Uhuru wa nchi hizo wakishirkia na nchi ya Tanzania, waliutumia katika kufanyia harakati zao.
Pichani
Wanajeshi na wanaharakati wa vita vya Msumbiji msituni Farm17 wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Wanajeshi na wanaharakati wa vita vya Msumbiji msituni Farm17 wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Hii picha ambayo inakuletea mwanga au inakupa sura ya mapambano dhini ya Ukoloni.
Ambapo mpaka miaka ya 1975 nchi ya Msumbiji ilifanikiwa kupata uhuru wake kutoka kwa Wareno.
Kwa Watu wa Msumbiji wanatambua sana thamani ya Tanzania na mikoa ya kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi. Na hii ni kutokana na historia halisi ya maisha yao ziligusa maeneo hayo.
Na. Victor Richard(Msafiri Tanzania) ft. Mayuni Joseph. www.historiayaafrika.co.tz
0 Comments