Abushiri ibn Salim al-Harthi alikuwa kiongozi wa upinzani dhidi ya ukoloni wa Wajerumani katika maeneo ya Pangani na pwani ya Tanzania ya leo mnamo 1889 .
HALI YA MAENEO YA PWANI MWAKA 1888
Pwani za Tanganyika na Kenya pamoja na visiwa kama Unguja au Mafia vilikuwa chini ya utawala Omani tangu mwaka 1698 wakati Waomani waliwafukuza
Wareno kutoka Mombasa .
Mnamo 1840 Sultani Said bin Sultan alihamisha mji mkuu wa utawala wake kutoka Maskat kuja Zanzibar mjini. Alidai pia ubwana juu ya miji yote ya Waswahili ilikuwepo kwenye pwani. Hali halisi miji ya Waswahili ilijitegemea kwa kiasi kikubwa vilevile ma kabila ya pwani na kanda la bara lililopo karibu na pwani. Lakini kwa jumla wote walikubali aina ya utawala wa juujuu wa sultani.
Katika miji muhimu Sultani aliweka ma liwali au kumkubali mkubwa wa mji kuwa liwali wake. Liwali alikuwa na wajibu wa kukusanya ushuru kwa ajili ya sultani na hii ilikuwa muhimu hasa kwa ma bandari ambako watumwa na pembe za ndovu walifanyiwa biashara .
Sultani wa Zanzibar alidai pia namna ya utawala kuhusu sehemu za ndani zaidi, hasa katika eneo la
njia za misafara baina ya pwani na Tabora - Ujiji - Ziwa Tanganyika . Lakini usultani haukuwa na
mamlaka halisi hapa isipokuwa penye maboma ya Waswahili au Waarabu na misafara yao.
Kwa kipindi kifupi Tippu Tip aliweza kuunganisha wafanyabiashara Waarabu katika mashariki ya Tanganyika na magharibi ya Kongo kukubali kwa jina ukuu wa Sultani wa Zanzibar.
KUFIKA KWA WAJERUMANI.
Mnamo 1884 Mjerumani Karl Peters alifika Zanzibar akiwa mwakilishi wa Shirika kwa Ukoloni wa Kijerumani akaendelea kuvuka bahari na kufanya mikataba ya ulinzi na machifu kadhaa wa Tanganyika akiwemo Chifu Mangungo wa Msovero Kilosa. Hakujaribu kufanya mikataba katika eneo la pwani lenyewe ilhali alijua ilikuwa eneo la Kizanzibari. Hata hivyo sultani alipinga mikataba akidai ya kwamba machifu hao waliwahi kukubali ukuu wake, kwa hiyo Peters alikuwa alivunja eneo la Kizanzibari.
Lakini serikali ya Ujerumani, iliyowahi kupinga mipango ya Peters, hatimaye ilikubali na kutoa
waraka wa ulinzi kwa ajili ya maeneo ya mikataba ya Peters. Serikali ya Sultani ilipokataa kukubali madai yale ililazimishwa kuvumilia kwa kufika kwa manowari wa Kijerumani mbele ya mji wa Zanzibar.
Lakini madai ya Wajerumani juu ya sehemu za bara zilikuwa bure kama pwani yote ilikuwa chini ya Sultani na bidhaa zote zilifika au kutoka katika maeneo haya zilipaswa kupitia mabandari ya sultani na kupigwa ushuru hapo.
Mwaka 1886 Uingereza na Ujerumani zilipatana kati yao kugawa maeneo ya bara na wakati uleule walitambua eneo la sultani kwenye bara kuwa kanda lenye upana la maili 10 pekee kuanzia mto Ruvuma hadi Mogadishu.
Sultani Bargash alipaswa kukubali kwa huzuni.
Uingereza iliahidi kumshawishi sultani ili kampuni ya Kijerumani ipate haki ya kutumia Pangani na Dar es Salaam (zilizokuwa katika eneo la sultani) kama mabandari yake. Sultani Bargash hatimaye alikubali yote kwa matumaini ya kuwa na hakika zaidi juu ya eneo lake.
Lakini mwaka uliofuata ambao ni 1887 tayari alikubali dai la Uingereza kukodisha pwani ya Kenya kwa shirika la Kiingereza la IBECO baadaye alianza kushauriana na Karl Peters juu ya mkataba wa aina hiyohiyo. Mkataba huu ulikwisha kusainiwa na mfuasi wake sultani Khalifa bin Said mnamo mwaka 1888.
Kufutana na mkataba kampuni ya Kijerumani ilipokea haki ya kusimamia kanda la pwani kati ya mto Ruvuma hadi Vanga kwa jina la sultani. Eneo hili lingeendelea kuwa sehemu ya Zanzibar na chini ya sheria ya Zanzibar, Kampuni ingetawala ushuru na kuwa na haki ya kuanzisha makazi na ma shamba au vituo vingine vya kiuchumi katika eneo hili. Sultani aliona faida ya kwamba angepata mapato ya kutegemea na Wajerumani jinsi alivyopata na Waingereza bila haja ya kumbuana na wakazi wa pwani.
Mapatano yalianza kutekelezwa mnamo Agosti 1888. Wenyeji wa pwani, ambao hawakuulizwa, wakashtuka walipoona maafisa Wajerumani waliofika na kupandisha bendera yao kando ya bendera ya sultani. Walishtuka zaidi juu ya ukali walioonyesha wawakilishi wa kampuni ya Kijerumani.
CHOKOCHOKO ZILIPOANZA KUSHIKA MOTO.
Uasi ulianza Pangani ambako wawakilishi wa Wajerumani walikataza kuonyeshwa kwa bendera ya Sultani na kudai kodi kubwa kwa bidhaa walipojaribu kutumia mamlaka yao. Wananchi waliwakamata na kuwafunga, lakini waliokolewa na jeshi la Sultani.
Huko Tanga Wajerumani walifungwa pia na kuokolewa na wanajeshi Wajerumani wa manowari ndogo iliyojulikana kama "SMS Moewe".
Tarehe 22 Septemba watu wa Bagamoyo walishambulia boma la Wajerumani lakini walizuiliwa na silaha za manowari maarufu kama "Leipzig".
Boma liliendelea kushambuliwa.
UASI ULIENDELEA KUPAMBA MOTO HADI PWANI YA KUSINI.
Hapa Abushir akiwa na majemadari wake.
Uasi ulienea kusini mnamo 25 Septemba 1888. Ma afisa wa kampuni katika Kilwa Kivinje waliuawa. Wajerumani walikimbia kutoka Lindi na Mikindani .
Katika Januari 1889 wamisionari Wakatoliki watatu waliuawa huko Pugu / Dar es Salaam .
KUSHINDWA KWA KAMPUNI YA KIJERUMANI NA KUINGILIA KWA SERIKALI.
Meja von Wissmannm jemadari wa serikali ya Ujerumani aliyefaulu kukomesha upinzani ya Abushiri
Kampuni ilishindwa kukandamiza upinzani huo ikaomba serikali ya Berlin kuingilia kati.
Serikali ilichukua koloni mikononi mwake. Wanamaji wa manowari za Ujerumani zilizokaa katika Bahari Hindi walifika Bagamoyo na Dar es Salaam wakafaulu kutetea vituo hivyo dhidi ya mashambulio.
Afisa Mjerumani Hermann von Wissmann aliagizwa kukusanya jeshi akipewa makisio ya milioni 2;
Wissmann aliajiri maafisa 21 na ma afande 40 kutoka Ujerumani akaelekea Afrika.
Njiani alipitia Misri akawaajiri askari Wasudan 600 kutoka jeshi la Misri (walioachishwa kazi wakati ule kutokana na kupungukiwa kwa jeshi la Misri baada ya vita ya Mahdi ).
Baadaye askari 150 Wazulu waliajiriwa katika
Msumbiji kama nyongeza.
Jeshi hilo lilijulikana kama "Wissmanntruppe" (kikosi cha Wissmann). Walipewa usaidizi na manowari za Kijerumani zilizokaa katika Afrika ya Mashariki.
Kikosi hicho kilichokuwa na silaha za kisasa kama
mabomu kilifaulu kukomesha upinzani wa wenyeji wa pwani.
Kwa jumla ma kabila ya bara hayakushiriki sana katika vita ya watu wa pwani.
Kikosi cha Wissmann kilibadilika baadaye kuwa
Schutztruppe yaani jeshi la kikoloni la serikali ya Ujerumani.
MWISHO WA VITA.
Picha hiyo juu ikimuonyesha shujaa Abushir akiwa chini ya ulinzi wa askari wa kijerumani.
Abushiri alikamatwa na kunyongwa tarehe 16 Desemba 1889 . Kufikia Agosti 1889 vita ilikuwa imekwisha.
Eeno la awali la kampuni likawa koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
0 Comments