Huenda kwa machache Liberia unaikumbuka kwa majina kama Charles Taylor na Samwel Sajenti Doe, na zaidi sana George Opong Weah......Kuna Mengi Huenda Huyajui Kuhusu Liberia

1. Liberia na Sierra Leone ni nchi mbili pekee duniani zilizoanzishwa na kudhibitiwa na Ukoloni hivyo kuendelea kuakisi dhana ya uhuru wa bendera. Lengo kuu kwa nchi hizi ilikua ni ziwe dampo la watu weusi wanaoachwa kwa sababu mbalimbali huko ughaibuni na hasa watumwa na watu wasio na tija (wachovu, wafungwa sugu, watukutu na fukara wa kupindukia) na hili hasa lilitokea baada ya Mapinduzi ya viwanda ambapo mashine zilianza kutumika kama mbadala wa kazi zilizofanywa na watu/watumwa 

2. Liberia Kimsingi Haijawahi kuwa chini ya Ubedui ingawa kimsingi imekua Bedui tangu kuanzishwa kwake kwani ilianzishwa na Chama cha Kikoloni cha Marekani na hapo ndipo eneo lililotengwa kwa ajili ya watumwa walioachiwa huru na ndio maana ya neno Liberia yaani The Land of The Free na hata Mji mkuu wa nchi hiyo Monrovia unaakisi jina la Rais wa Marekani Monroe James kadhalika Katiba na Muundo wa Serikali ( For 133 years, Liberia is ruled by the True Whig Party, whose government and constitution are modeled after the United States.)

3. Bendera ya Liberia Inashabihiana sana na Ile ya Marekani ingawa na ile michirizi kumi na moja inatajwa kama ni kiwakilishi cha watu 11 waliosaini mkataba wa uhuru (bendera) lakini kuna mengi nyuma ya pazia hasa kwa hiyo nyota moja

4. Ni miongoni mwa nchi chache Afrika ambapo karibu makabila yote yanapatikana na hii ni kutokana na ukweli kwamba nchi hiyo ilikua kama dampo la watumwa walioachiwa huru na kasi iliongezeka baada ya Mapinduzi ya Viwanda

5. Historia ya Liberia inashabihiana kidogo na Sierra Leone (Lion Mountains) yenye mji pia unaoitwa Free Town, ingawa Sierra Leone (The Province of Freedom) yenyewe ilikua dampo la waingereza masikini ( London's "Black Poor" Province) na ndio maana nchi hiyo ina machotara wengi
6. Licha ya Kuongozwa na Rais mwanamke wa kwanza kabisa Afrika (Iron Lady), Nchi hiyo ina wabunge 13 tu wanawake kati ya wabunge wote 103 sawa na asilimia 13 tu.  Kama hiyo haitoshi, mwanamke wa kwanza kuingia jeshini ilikua ni mwaka 2006 

7. Kwa Mujibu wa makadirio ya idadi ya watu ya mwaka 2015, Jumla ya Watu wote Liberia ni sawa na Idadi ya Watu wote wa Dar Es Salaam, ongezeko dogo sana la watu linaathiriwa sana na wazamiaji wa ulaya na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa miaka mingi (14) na kuua maelfu ya watu (zaidi ya makumi elfu ya watu kati ya mwaka 1989-2003) hapa mapigano kati ya waliojiita wenyeji akina Samuel Doe (Krahn ethnic group) dhidi ya walioitwa wageni toka uhamishoni akina Charles Taylor.