Ziwa masoko au Kisiba linapatikana mkoani Mbeya katika wilaya ya Rungwe itakuchukua kilomita 19 mpaka ulifikie kama ukitokea Tukuyu Mjini.
Kuna masimulizi mengi kuhusu Ziwa hili, mengi yakiwa ya Kitamaduni zaidi na hii ndiyo huvutia watu wengi kwenda kutalii katika ziwa hilo.
Inaaminika kuwa kipindi Wajerumani katika vita ya kwanza ya Dunia wakati wanaondoshwa walitupia mali nyingi sana katika ziwa hilo. Karibu na ziwa hilo la Kisiba kuna eneo ambalo linaitwa Bomani ambapo hapo utakuta makaburi matatu ya Wajerumani.
Kwa mujibu wa Simulizi unaambiwa kuwa Makaburi hayo ni makumbusho kwa Wajerumani waliokufa kipindi walipokuwa wanaondolewa katika Vita ya kwanza ya dunia.
Lakini zaidi inaongezwa pia katika eneo hilo kuna ugomvi ulitokea kati ya nyoka mkubwa aliyekuwa na vichwa viwili na mjerumani mmoja. Inaaminika pia katikati ya maji kuna nyoka mkubwa ambae amezunguka chungu ambacho kimejaa Rupia’.
Watu kadhaa hujaribu kuchukua Rupia hizo lakini hakuna aliyewahi kufanikiwa zaidi ya wengine kupoteza mpaka maisha. Inaelezwa zaidi kuwa Kila ifikapo saa 12 jioni kuna mstari hupita kwa kasi kuelekea katika makaburi ya Wajerumani upande wa Bomani’
Mstari huo hupita kwa kasi kubwa sana kiasi kwamba kama hautakuwa makini basi utashuhudia unavyogawanyika tu.
0 Comments