Hii hapa ni historia fupi ya taifa la Uganda.



Hii hapa ni historia fupi ya taifa la Uganda.
1500 – Falme za Buganda, Bunyoro na Ankole zaanzishwa na watu wa ukoo wa Bito, wa Waniloti, wenye asili ya kusini mashariki mwa Sudan.
1700 - Buganda yaanza kupanuka na kutwaa maeneo ya Bunyoro.
1800 - Buganda yadhibiti maeneo yaliyo kati ya Ziwa Victoria na Mto Nile na Mto Kagera.
1840s – Wafanyabiashara wa Kiislamu kutoka pwani ya Bahari ya Hindi wafika na kuuzia Buganda bunduki, nguo na shanga. Wachukua pembe na watumwa kutoka Buganda.
1862 – Mwingereza John Hanning Speke awa Mzungu wa kwanza kufika Buganda.
1875 – Mfalme wa Buganda King Mutesa I awaruhusu wamishenari Wakristo waingie ufalme wake.
Utawala wa Uingereza
1877 – Wamishenari wa British Missionary Society wawasili Buganda.
1879 – Wamishenari wa French Roman Catholic White Fathers wawasili.
1890 – Uingereza na Ujerumani zatia saini mkataba wa kukabidhi Uingereza haki ya kusimamia maeneo ambayo sasa ni Uganda.
1892 – Wakala wa kampuni ya Imperial British East Africa Frederick Lugard apanua udhibiti wa kampuni hiyo hadi kusini mwa Uganda na kuwasaidia wamishenari waprotestanti kuwazidi wenzao Wakatoliki katika maeneo ya Buganda.
1894 - Uganda yafanywa kuwa nchi lindwa ya Uingereza.
1900 – Uingereza yatia saini makubaliano na Buganda ya kuupa ufalme huo uhuru kiasi na kuufanya kuwa ufalme wenye misingi ya kikatiba ambao unadhibitiwa sana na machifu Waprotestanti.
1902 – Mkoa wa mashariki wa Uganda wahamishiwa Kenya.
1904 – Ukulima biashara wa pamba waanza.
1921 - Uganda yaundiwa baraza la kuunda sheria, lakini mbunge wa kwanza Mwafrika alikubaliwa 1945.



1958 - Uganda yapewa uhuru kiasi.
1962 - Uganda yapata uhuru kamili Milton Obote akiwa waziri mkuu na Buganda ikiwa na uhuru mwingi.
1963 - Uganda yawa jamhuri huku Mfalme Mutesa wa Buganda akiwa Rais.
1966 - Milton Obote amaliza uhuru wa Buganda na kujifanya rais.
1967 – Katiba mpya yampa rais madaraka makubwa.
Miaka ya Idi Amin
1971 – Milton Obote aondolewa madarakani na kiongozi wa majeshi Idi Amin.


Amin
Image captionIdi Amin Dada

1972 - Amin awaagiza Wahindi wote ambao hawakuwa raia wa Uganda, takriban watu 60,000, waondoke nchini humo.
1972-73 - Uganda yakabiliana mara kwa mara na Tanzania mpakani.
1976 - Idi Amin ajitangaza kuwa kiongozi wa daima na kudai baadhi ya maeneo ya Kenya.
1978 - Uganda yaivamia Tanzania ikilenga kutwaa mkoa wa Kagera.
1979 - Tanzania yaivamia Uganda, yaunganisha makundi yaliyompinga Amin chini ya Uganda National Liberation Front na kumlazimu Amin kukimbia nchi; Yusufu Lule akabidhiwa urais, lakini muda mfupi baadaye nafasi yake inachukuliwa na Godfrey Binaisa.
1980 - Binaisa anapinduliwa na jeshi.
Milton Obote anakuwa rais baada ya uchaguzi.
1985 - Obote anapinduliwa na jeshi na nafasi yake kuchukuliwa na Tito Okello.
1986 – Wapiganaji wa National Resistance Army wateka Kampala na kumuweka Yoweri Museveni kwenye uongozi.


MuseveniHaki miliki ya pichaAP
Image captionBw Museveni
Mwanzo wa kujikwamua
1993 - Museveni arejesha wafalme wa kijadi, ukiwemo ufalme wa Buganda, lakini bila nguvu za kisiasa.
1995 – Katiba mpya inatoa nafasi ya kuundwa kwa vyama vya kisiasa lakini marufuku ya shughuli za kisiasa inaendelea kuwepo.
1996 - Museveni ashinda uchaguzi wa kwanza kamilifu wa urais nchini Uganda.
1997 – Wanajeshi wa Uganda wasaidia kumuondoa madarakani Mobutu SeseSeko wa Zaire, ambaye nafasi yake inachukuliwa na Laurent Kabila.
1998 – Wanajeshi wa Uganda waingilia kijeshi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (iliyojulikana kama Zaire) wakiunga mkono waasi waliotaka kumuondoa madarakani Kabila.
2000 – Raia wa Uganda wapiga kura kukataa siasa za vyama vingi na badala yake kuunga mkono mfumo wa Museveni wa “kutokuwa na chama”.
2001 Januari – Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yazinduliwa mjini Arusha, Tanzania, na kuweka msingi wa kutumiwa kwa pasipoti na bendera ya pamoja Afrika Mashariki pamoja na kufungamanisha mifumo ya kiuchumi na kifedha. Wanachama ni Tanzania, Uganda na Kenya.
2001 Machi - Uganda yaiorodhesha Rwanda, mshirika wake wa zamani katika vita vya wenyewe kwa wenyewe DR Congo, kama taifa adui kutokana na kupigana kwa majeshi ya mataifa hayo mawili Dr Congo 2002.
Museveni ashinda uchaguzi kwa mara nyingine, akimshinda mpinzani wake mkuu Kizza Besigye kwa 69% dhidi ya 28%.
Kukabiliana na waasi
2002 Machi - Sudan, Uganda zatia saini mkataba wa kukabili waasi wa Lord's Resistance Army (LRA) kutoka Uganda, ambao walikuwa wakiendesha shughuli zao katika mapaka kati ya nchi hizo mbili.


Kony
Image captionJoseph Kony

2002 Oktoba – Jeshi lawahamisha zaidi ya raia 400,000 waliokuwa maeneo yaliyoathirika zaidi na vita vya LRA, waasi ambao wanaendelea kushambulia vijiji kwa ukatili mkubwa.
2002 Desemba – Mkataba wa amani watiwa saini kati ya serikali na waasi wa Uganda National Rescue Front (UNRF) baada ya mazungumzo ya zaidi ya miaka mitano.
2003 Mei - Uganda yaondoa wanajeshi wake wa mwisho kutoka mashariki mwa DR Congo. Maelfu ya raia wa DR Congo watafuta hifadhi Uganda.
2004 Februari – Waasi wa LRA waua zaidi ya watu 200 katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Uganda.
2004 Desemba – Serikali na waasi wa LRA wafanya mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana, lakini hakuna mwafaka unaopatikana.
2005 Aprili - Uganda yakataa madai yaliyotolewa na DR Congo katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) mjini The Hague. DR Congo ilidai Uganda ilivamia ardhi yake 1999 na kuua raia pamoja na kupora mali.
Siasa za vyama vingi
2005 Julai – Bunge laidhinisha katiba ambayo inaondoa kikomo cha mihula miwili kwa rais.
Wapiga kura waidhinisha kurejelewa kwa siasa za vyama vingi kwenye kura ya maamuzi.
2005 Oktoba – Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) yatoa vibali vya kukamatwa kwa makamanda watano wa LRA, akiwemo kiongozi Joseph Kony.
2005 Novemba – Kiongozi mkuu wa upinzani KizzaBesigye azuiliwa kwa muda baada ya kurejea kutoka uhamishoni baada yake kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi kujibu mashtaka kadha yakiwemo uhaini na umiliki wa siasa. Wafuasi wake wasema kesi hiyo ni ya kisiasa, na kuandamana barabarani. Besigye aliachiliwa huru kwa dhamana Januari 2006, muda mfupi kabla ya uchaguzi wa urais.
2005 Desemba – Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague yaamua Uganda ni sharti ilipe fidia DR Congo kwa makosa ya ukiukaji wa haki za kibinadamu na uporaji wa rasilimali wakati wa vita vya miaka mitano hadi 2003.


BesigyeHaki miliki ya pichaBBC WORLD SERVICE
Image captionDkt Kizza Besigye

2006 Februari - Rais Museveni ashinda uchaguzi wa vyama vingi, akipata 59% ya kura dhidi ya 37% za mpinzani wake mkuu, Kizza Besigye. Waangalizi wa uchaguzi kutoka EU wataka kuhangaishwa kwa Besigye na vyombo vya habari vya serikali kupendelea serikali kama kasoro.
2006 Agosti – Serikali na LRA watia saini mkataba wa kusitisha mapigano. Mazungumzo ya amani yaliyofuata yakumbwa na misukosuko, washiriki wakijiondoa mara kwa mara.
2006 Novemba – Serikali yapuuzilia mbali ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyolituhumu jeshi kwa kutumia nguvu kupita kiasi katika kukabiliana na kupokonya silaha wapiganaji katika eneo la kaskazini mashariki la Karamoja.
Mchango Somalia
2007 Machi – Uganda yatuma walinda amani Somalia chini ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika kusaidia kurejesha uthabiti nchini humo.
Shirika la Chakula Duniani (WFP) lasema litalazimika kupunguza kwa nusu misaada ya chakula kwa zaidi ya watu 1 milioni walioachwa bila makao kutokana na vita kaskazini mwa Uganda.
2007 Aprili – Maandamano kuhusu msitu yababisha ghasia za ubaguzi wa rangi, na kuwalazimu polisi kutumia nguvu kulinda biashara za Wahindi na hekalu la Wahindi. Mwanamume Mhindi na watu wengine wawili wauawa.
2007 Juli - Lord's Resistance Army wasema ukosefu wa pesa za kusafiri nje na kufikia makamanda mafichoni vitachelewesha mazungumzo.
2007 Agosti - Uganda na DR Congo zakubali kutatua mzozo mpakani.
2007 Septemba – Hali ya dharura yatangazwa baada ya mafuriko kusababisha uharibifu mkubwa.
2008 Februari – Serikali na waasi wa Lord's Resistance Army watia saini mkataba wa kudumu wa kusitisha mapigano Juba, Sudan.
2008 Novemba – Kiongozi wa Lord's Resistance Army, Joseph Kony, kwa mara nyingine akosa kujitokeza hafla ya kutiwa saini kwa mkataba wa amani. Wanajeshi wa Uganda, Sudan Kusini na DR Congo waanza operesheni dhidi ya kambi za LRA.
2009 Januari - Lord's Resistance Army waitisha mkataba wa kusitisha mapigano kufuatia operesheni kali iliyotekelezwa na majeshi ya kanda.
Shirika la kupeleleza mafuta kutoka Uingereza la Heritage Oil lasema limegundua kiasi kikubwa cha mafuta Uganda.
2009 Machi – Wanajeshi wa Uganda waanza kujiondoa DR Congo, maeneo ambayo walikuwa wameingia kuwasaka waasi wa Lord's Resistance Army.
2009 Oktoba – Wapiganaji wa al-Shabaab kutoka Somalia watishia kushambulia Uganda na Burundi baada ya shambulio la walinda amani wa Umoja wa Afrika Somalia kusababisha vifo vya raia kadha.
2009 Desemba – Bunge lapiga marufuku ukeketaji wa wasichana. Laidhinisha adhabu ya miaka 10 jela au kufungwa jela maisha mwathiriwa wa ukeketaji akifariki.
2010 Januari - Rais Museveni ajitenga na sheria ya kuharamisha mapenzi ya jinsia moja, akisema mbunge wa chama tawala aliyewasilisha mswada huo aliuawasilisha kama mtu binafsi. Umoja wa Ulaya na Marekani walikuwa wameshutumu mswada huo.
Jeshi la Uganda lasema limemuua Bok Abudema, kamanda mmoja mkuu wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
2010 Februari - Heritage Oil yauza mali yake Uganda kwa kampuni ya Uingereza ya Tullow Oil baada ya kampuni ya Eni kutoka Italia kujiondoa.
2010 Juni – Mwendesha mashtaka wa umma aanzisha uchunguzi wa tuhuma za ufisadi dhidi ya makamu wa rais Gilbert Bukenya, waziri wa mashauri ya kigeni Sam Kutesa na mawaziri wengine kadha pamoja na maafisa wakuu serikali kuhusiana na kutoweka kwa $25m.
2010 Juni-Agosti - Opereshenu Rwenzori dhidi ya waasi wa ADF-NALU waliokuwa wakipigania kuunda kwa taifa la Kiislamu Uganda yasababisha watu 90,000 kutoroka makwao mkoa wa Kivu Kaskazini katika nchi jirani ya DR Congo.
Milipuko
2010 Julai – Mashambulio mawili ya mabomu watu wakitazama fainali ya Kombe la Dunia mgahawani na katika kilabu ya raga mjini Kampala yaua watu 74. Kundi la al-Shabab kutoka Somalia ladai kuhusika.
2010 Agosti – Uchaguzi wa mchujo wa chama cha National Resistance Movement wa kuteua wagombea ubunge na udiwani wasimamishwa kutokana na udanganyifu na ghasia.
2010 Okktoba – Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuuawa kwa Wahutu DR Congo kati ya 1993 na 2003 yasema huenda ni “makosa ya mauaji ya halaiki”. Yatuhumu Rwanda, Uganda, Burundi, Zimbabwe na Angola.
2010 Oktoba – Mahakama ya Kikatiba yatupilia mbali mashtaka ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.
2011 Februari - Museveni ashinda uchaguzi wa kuongoza kwa muhula wa nne. Mpinzani wake Kizza Besigye adai kulikuwa na wizi wa kura na kupuuzilia mbali matokeo.
2011 Aprili – Kizza Besigye akamatwa mara kadha kuhusu maandamano yake ya ''walk-to-work'' (kutembea kwenda kazini) kulalamikia kupanda kwa bei za bidhaa na huduma.
2011 Julai – Marekani yatuma vikosi maalum kusaidia Uganda kukabiliana na waasi wa LRA.
2011 Septemba – Mahakama yaamuru kuachiliwa huru kwa kamanda wa LRA Thomas Kwoyelo, na kusema anafaa kupewa msamaha na serikali.
2012 Mei – Jeshi la Uganda lamkamata mmoja wa makamanda wakuu wa LRA Caesar Achellam wakati wa mapigano jamhuri ya Afrika ya Kati, moja ya mataifa ambayo bado yanatatizwa na wapiganaji wa LRA. Uganda yasema ni hatua kubwa, na kusema Achellam alikuwa mpangaji mikakati wa LRA.
Maelfu ya wakimbizi waingia Uganda, wakitoroka mapigano DR Congo.
Madai DR Congo

Uganda
Image captionUganda ilijipatia uhuru wake 1962

2012 Julai – Umoja wa Mataifa waituhumu Uganda kwa kutuma wanajeshi DR Congo wakasaidie wapiganaji wa M23, tuhuma ambazo Uganda inakanusha.
2012 Novemba - Uganda yatangaza nia ya kujiondoa kutoka kwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa kulalamikia tuhuma zilizotolewa na UN kwamba inasaidia waasi Congo.
Uingereza na nchi nyingine za Ulaya zasitisha ufadhili ambao ulituwa ukipitia kwa serikali ya Uganda kutokana na tuhuma za wizi wa fedha kutoka kwa wafadhili.
2013 Februari – Mataifa kumi na moja, ikiwemo Uganda, yatia saini mkataba uliofanikiwa na Umoja wa Mataifa wa kutoingilia hali DR Congo.
2013 Machi - Uganda yawekwa pamoja na mataifa yanayohusika sana katika biashara haramu ya pembe za ndovu katika mkutano wa CITES, shirika linalodhibiti biashara ya wanyamapori.
2013 Mei – Serikali yafunga kwa muda magazeti mawili yaliyochapisha barua inayoonyesha huenda Rais Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume awe mrithi wake.
2013 Novemba – Baraza la Kampala lamtoa madarakani meya wa chama cha upinzani cha Democratic Party Erias Lukwago kutokana na tuhuma za kutomudu kazi na kutumia vibaya mamlaka. Chama cha Democratic Party chaituhumu serikali kwa kupanga njama ya kumuondoa kiongozi huyo pekee wa upinzani aliyekuwa na wadhifa mkuu zaidi.
2013 Desemba – Bunge lapitisha sheria tata ya kuongeza adhabu dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ikiwemo kufungwa jela maisha.
2014 Februari – Rais Museveni atia saini mswada tata wa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja, hatua iliyoshutumiwa vikali na viongozi wengi duniani.
Benki ya Dunia yaahirisha utoaji wa mkopo wa $90m (£54m) kwa Uganda kutokana na hatua hiyo, Marekani nayo yaiwekea Uganda vikwazo.
2014 Julai – Watu karibu 100 wafariki kwenye makabiliano kati ya jamii pinzani na jeshi eneo la Rwenzori magharibi.


Bw MbabaziHaki miliki ya picha
Image captionBw Amama Mbabazi

2014 Septemba - Rais Museveni amfuta kazi waziri mkuu Amama Mbabazi.
2014 Desemba – Jenerali mtoro David Sejusa, aliyekosana na Rais Museveni, arejea ghafla kutoka uhamishoni.
Zaidi ya wapiganaji 1000 wa zamani wa kundi la waasi la M23 nchini DR Congo waomba hifadhi nchini Uganda baada ya serikali kujaribu kuwarejesha nchini mwao.
Wahubiri wawili wa Kiislamu wauawa na watu wanaoendesha pikipiki. Polisi washuku wapiganaji wa Allied Democratic Forces, wanaopigania kuundwa kwa dola ya Kiislamu, waliwaua wawili hao kwa kutowahimiza watu kujiunga na kundi hilo.
2015 Januari - Dominic Ongwen awa mwanachama wa kwanza kwa Lord's Resistance Army kufikishwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita.
2015 Machi – Kesi dhidi ya watu 13 wanaotuhumiwa kuhusika mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na al-Shabaab Kampala 2010 yasimamishwa baada ya mwendesha mashtaka mkuu katika kesi hiyo kufariki.
2015 Mei – Waasi wa Allied Democratic Forces kutoka Uganda watuhumiwa kutekeleza mauaji eneo la Beni katika taifa jirani la DR Congo.


OngwenHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionDominic Ongwen akiwa mahakama ya ICC

2015 Juni – Waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi asema atakabiliana na mshirika wake wa zamani, Rais Museveni, katika uteuzi wa mgombea urais wa chama tawala cha National Resistance Movement.

Post a Comment

0 Comments