Kuna mambo mengi ya kusisimua ya harakati za kupigania uhuru wa nchi za Afrika labda hayajapata kabisa kusimuliwa au simulizi zake hazijapewa nafasi ya kutosha kulinganisha na ukubwa wa masimulizi hayo.Mfano kuvalishwa kwa baibui kwa Hayati baba wa taifa Mwl Julius Nyerere na Kitwana Kondo kumuepusha na polisi.
Marehemu Kitwana alifanya hivi mwaka 1958 wakati chama cha TANU kilipokua kwenye mkutano wake katika jengo la klabu ya Yanga mtaa Mafia.Kwenye mkutano huo uliokua wa jinsia zote,kulikua na milango miwili ya kutumika kulingana na jinsia.Mwalimu alipitishwa mlango uliokua unatumiwa na wakina mama huku akivalishwa baibui kuwakwepa askari wa kikoloni waliokua wanamsubiri mlango wa wanaume.
Katika uchache huo ama kutopata nafasi ya kutosha au kutosimuliwa kabisa,Kongwa ni moja wa maeneo yaliyoathirika kutokana na kupunjwa hadhi yake ya kuhistoria wakati wa harakati za kupigania uhuru wa bara la Afrika hasa kwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
Mwaka1963 ,iliundwa kamati ya ukombozi ya iliyokua Umoja wa nchi huru za Afrika(OAU).Tanzania ikawa kituo cha wapigania uhuru na mafunzo ya kijeshi.Eneo la Kongwa(sasa ni wilaya)kikawa kituo cha cha mafunzo hayo kilichopokea wapigania Uhuru toka nchi za Msumbiji,Namibia,Zimbabwe,Angola,Afrika ya Kusini na nyinginezo zilizipo chini ya jangwa la Sahara.
Kuna sababu nyingi zilizoifanya Tanzania kuchagua eneo la Kongwa mkoani Dodoma kuwa kituo cha mafunzo ya kijeshi mojawapo ni ni miundombinu ikiwepo reli iliyotoka Msagali hadi kituo cha Kongwa na Hogoro.Reli hiyo ilijengwa sambamba na nyumba za watumishi wa wa shirika hilo.Moja ya nyumba hizo ilikuja kutumika na ayekua rais wa Kwanza wa Msumbiji Samora Macheli aliyekua miongoni mwa wapigania uhuru waliopo katika kituo hiko cha Kongwa.
Ujenzi wa reli hiyo ulitokana na kukua kwa kilimo cha karanga kilochokua kikiendeshwa na shirika la Overseas food production la wazungu kama mkakati wa kiuchumi wa kufufua uchumi wa waingereza baada ya kuathirika na vita kuu ya pili ya dunia.
Ukiacha reli,nyumba kilimo hiko pia kilichangia kwa kiasi kikubwa kulifanya eneo la lote la Kongwa kutambulika rasmi kama wilaya ndogo mwaka 1947Pia ujenzi wa shule ya sekondari ya watoto wa waingereza ya Kongwa European School iliyokuja kuhamishiwa mkoani Iringa mwaka 1960 kabla ya kutaifishwa na serikali na kua Mkwawa High School.
Wakiwa Kongwa wapigania hao uhuru akiwemo aliyekua rais wa kwanza wa Namibia Samueli Shafiishuna Daniel Mujoma maarufu kama Sam Mujoma walijifunza tamaduni mbali za wagogo.
Mujoma aliyeingia Kongwa kupitia Njombe,Iringa alijifunza kuongea kigogo wakati rais wa kwanza Msumbiji,Samora Machel alifanya kazi kama mganga msaidizi huku baadhi ya askari wakifika vijijini na kunywa pombe za kienyeji na wenyeji wa Kongwa zikiwemo primisi inayotengenezwa kwa mchuzi wa Tangawizi na Choya inayotokana na juice ya tunda la Alover.
Ukiacha sababu ya miundo mbinu,jiografia ya Kongwa pia ilichangia eneo hilo kutumika kama kituo cha mafunzo hasa safu za milima Mlanga ilyotumika katika mafunzo ya kijeshi.Licha ya Samu Mujoma wapigania uhuru wengine waliopata mafunzo Kongwa ni pamoja na Rais wa sasa wa Namibia Ifike Pohamba,Mose Tjitendero.
Msumbiji ni moja ya nchi zinazozndelea mpaka sasa kua na desturi ya kuienzi Kongwa.Mpaka sasa nchini humo inaaminika mtu anayetaka kugombea nafasi ya urais wa nchi hilo kupitia chama cha Flerimp,lazima afike Kongwa kupata baraka za ushindi.Maris Filipe Nyusi na Armando Guebuze wote wamefika Kongwa kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais wa nchi hiyo.
Sambamba na hilo ncho hiyo iliyopata uhuru wake juni 25,1975 inakumbukwa na wakazi wa Kongwa kwa maisha aliyoishi rais wa kwanza wa nchi hiyo Samora Machel.Samora anakumbukwa na wakazi wa Kongwa kwa uchezaji mpira.Alikua msakata kabumbu mzuri tu wakati huo akijichanganya na timu za wanakijiji kiasi cha kukumbukwa na wakazi wa Kongwa wa wakati huo ambao wengi kwa sasa ni wazee.
Lakini pia uwepo wa andaki ambalo mpaka wakati huu linatumika kama kumbukumbu ya alama ya wapigania uhuru.Andaki hilo refu linalokadiriwa kua na kimo cha meta tano kwenda chini na upana unaoruhusu mtu mmoja kutembea,kwa sasa limebomoka kwenye mlango wa kuingilia,lilitumiwa na rais huyo wa kwanza wa Msumbiji kujificha wakati wa harakati zake,lipo
umbali wa mita takribani mia tano kutoka katika nyumba aliyokua akiishi Samora Machel.Limejengwa kwa saruji imara kuna ngazi za kuingilia na kutokea upande wa pili.
Kabla ya uhuru Kongwa ilikua ikiongozwa na watemi na machifu.Mfano eneo la Panda mbili lilikua chini ya Mtemi Nyamanji,Mtemi Mahinyila alitawala eneo la Kongwa huku eneo lote la Mlale likiwa chini ya Kasuwa na Sagara ilikua chini Mtemi Simango.
Wakati huu unaposoma makala haya Kongwa ni moja kati ya wilaya saba za mkoa wa Dodoma.Kabla ya tarehe 23/6/1995 wilaya hii ilikua sehemu ya Wilaya ya Mpwapwa.Mipaka ya wilaya hiyo ilitangazwa rasmi kwenye gazeri la serikali la Novemba 8,1996 kwa tangazo Na 349.Wilaya hii sasa ina ukubwa wa kilometa za mraba 4,041,tarafa 3,kata 22,vijiji 74 na vitongoji 281.
Hii ndio Kongwa ambayo kwa wakati huu imetoa wanasiasa machachari kwenye siasa za Tanzania .Job Ngugai Masonenyi Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni mbunge wa jimbo la Kongwa na wengine wengi.
0 Comments