Habari na historia hii itajikita kufafanua mambo machache ya kihistoria hasa juu ya watu wa Afrika mashariki na namna wageni kutoka Dunia nje ya Afrika, walivyoleta athari katika vizazi vya Afrika Mashariki. Kuna mengi ya kujua ila machache ni haya.
Inafahamika kuwa wakazi wa mwazo kabisa wa visiwa vya Unguja na Pemba ni watu waliotoka Tanzania, Msumbiji, Kenya na sehemu zingine za ndani ya bara la Afrika Mashariki. Wengi wao walikuwa Wabantu kutokea Afrika Magharibi.
Ukirejea maandiko ya watu wa Misri na Ugiriki waliofika Afrika mashariki kabla ya miaka ya 1000. Wanasimulia habari za watu weusi(Wabantu) waliowakuta kwenye visiwa hivyo na hata wale walikuwa wakiishi Pwani. Na hata wale Waarabu wa kwanza waliofikia maeneo hayo kwenye miaka ya 600BK/BM na kuanzisha Himaya yao, Waliwakuta watu weusi wakiwa na miji yao na maisha yao.
Hapa ifahamike kuwa, jamii nyingi za kibantu zilishafika Afrika mashariki muda mrefu sana kwenye miaka ya 500BK/BM, kabla ya ujio wa wageni hapa Afrika mashariki . Kulikuwa na miji mingi iliyoendelea hata kabla ya ujio wa Wageni, japo ujio wao Ilichangia kwa asilimia 90 kukuza miji hiyo. Mji kama Kilwa, ni moja ya mji uliopata kukua hata kabla ya miaka ya 600.
Ifahamike kuwa watu wa kwanza kuanzisha utawala wao Afrika mashariki ni Waarabu waliopata kufika mnamo miaka ya 749-1000.
Na baadae kwenye miaka ya 1400 walikuja Wareno. Na wakaja tena Waarabu ambao walikuwa wakitawala Afrika mashariki mpaka miaka ya 1890, ambapo tunapata ujio wa Mataifa ya Ulaya na kuanzishwa kwa ukoloni.
Na baadae kwenye miaka ya 1400 walikuja Wareno. Na wakaja tena Waarabu ambao walikuwa wakitawala Afrika mashariki mpaka miaka ya 1890, ambapo tunapata ujio wa Mataifa ya Ulaya na kuanzishwa kwa ukoloni.
Ujio wa Wageni hawa ulileta athari kubwa sana kwa wakazi wa awali ambao ndio hao Wabantu. Kwani walizaliana na kupata uzao ulio mchanganyiko. Na kipindi cha Sultan Said, kulialikwa Wahindi na Wakomoro wengi kuja kisiwani Zanzibar. Ambao nao walizaliana na wakazi wa Kibantu na kuleta athari maeneo hayo. Kwa ujumla wageni hao walileta athari nyingi ikiwemo vita na mabalaa mengine
Labda kuna haja ya kufahamu kwa uchache vita kati ya Waarabu na Wareno. Mambo yalikuwa hivi, Kwa miaka mingi Waarabu walikuwa wanajihusisha na biashara na watu wa Afrika Mashariki. Na mara baada ya Wareno kufika maeneo hayo, Walitaka kuytawala, kitu ambacho Waarabu hawakuwa tayari. Hivyo, mnamo miaka ya 1624 kulikuwa na bwana mmoja aliyekuwa mtawala wa Omani wakati huo, alifahamika kwa jina la Nasir Bin Murshidi. Alianzisha vita na Wareno huko Omani na kufanikiwa kuwaondoa.
Kwa wakati wote huo Wareno walikuwa wameshatawala maeneo yote ya Pwani ya Afrika mashariki.
Na hivyo Waarabu waliamua kuanzisha vita kwa upande wa Afrika mashariki kwa lengo la kuwaondoa Wareno mnamo miaka ya 1652.
Na hivyo Waarabu waliamua kuanzisha vita kwa upande wa Afrika mashariki kwa lengo la kuwaondoa Wareno mnamo miaka ya 1652.
Na mwisho wa siku Waarabu walishinda vita hivyo na kuchukua maeneo yote ya Afrika mashariki isipokuwa maeneo ya Msumbuji ambapo Wareno waliachiwa kukaa hapo na kumiliki.
Hivyo mpaka kufikia miaka ya 1690, Waarabu walifanikiwa kutawala maeneo ya Unguja, Mombasa, Kilwa na miji mingine iliokuwa katika maeneo ya Pwani ya Afrika mashariki.
Kwa kipindi chote hiko Masultani wa Omani waliwatumia Maliwali kama wawakilishi waliokuwa wakisimamia maeneo hayo. Kwenye miaka 1700-1800, huko Omani kulitokea migogoro mingi kwa upande wa Masulatani waliokuwa huko. Na migogoro ilikuwa mingi hasa kile kipindi ambacho baba wa Sultani Sayyid Said alipokuwa mtawala. Na mara baada ya Uongozi huo Kurithishwa Sultani Sayyid Said, kulifanyika mabadiliko makubwa sana. Kubwa ni lile la kuhamishiwa kwa utawala huo kutoka Omani na Kuja Zanzibar 1830-1840.
Na ikumbukwe kuwa wakati wote huo kulikuwa na biashara ya Utumwa (iliokuwa ikifanywa na Wafaransa pamoja na nchi zingine za Ulaya bila kusahau nchi za Uarabuni).
Na idadi kubwa ya watu (Wabantu) walikuwa wanaenda Zanzibar ni watumwa. Watumwa walikuwa wakitumika kwa kazi za nyumbani, Mashambani pamoja na kwenye viwanda vidogovidogo. Kuna baadhi ya Waarabu walikuwa wakiwaoa Waafrika waliokuwa wakienda Zanzibar na hata kule Omani na kuzaa watoto. Na hapo kukawa na mazalia ya watoto kutoka Uarabuni na Afrika.
Hivyo makabila yaliyopo kule Unguja na Pemba ni machanganyiko wa watu mbalimbali. Yaani tunaweza kusema kuwa ni kizazi kilichotokana na kuingilian kwa makabila ya kibanti na Watu Bara la Asia.
👍Na ifahamike kuwa hapa ulimwenguni watu weusi wanatoka Afrika tu na sio kwingine. Kama Waafrika wapo sehemu hizo biashara ndio ilikuwa chanzo cha Waafrika kufika huko.
0 Comments