Kwa kutambua umuhimu wa mimi kuandika makala hii naomba kwanza kutambua kwa heshima kubwa sana kwa namna nilivyoshawishika kushika kalamu na kuanza kuiandika andiko hili katika ufansi yakinifu na upembuzi sanifu wa hari ya juu ni baada ya kupokea maoni kutoka kwa ndugu yangu wa karibu ndugu Jeremiah Caleb Odinga Celebu alipo niomba niaandae andiko juu ya umoja wetu wa Afrika. Sikusita na ndipo nakaamua kuiandaa makala hii iliyo nichukiwa siku tatu (3).
Afrika ni bara la pili kwa ukubwa katika sayali yetu yenye kuhifadhi viumbe hai ya dunia. Ambayo pamoja na kuwa na historia kuntu ya mda mrefu toka zama za kale za maisha ya mwanadamu (Athopithecus Africans) miaka 12 milioni BCE mpaka zama za Udurufu wa mwanadamu (Homo Sapieni) miaka 2 milioni BCE iliopita.
Toka zama hizo mpaka kipindi cha ustarabu wa dunia (World Civilazation) bara la afrika limekiwa likiishi kwa ufanisi mkubwa kabisa kwa kuenenda ustaarabu (world Civilazation) huu wakati wa zama za utawala wa Misiri (Egypt Empire).
Pamoja na kupitia changamoto nyingi za kihistoria kama utumwa, uvamizi na ukoloni wa kibeberu kwa mda mrefu hatimaye miaka ya 1960 hali ya kifikra katika Afrika ilianza kubadilika na kupelekea ukombozi wa kisiasa katika bala zima na kuibuka kwa hamasa za ukombozi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kitamaduni. Hamasa hii ilipeleka kuundwa chombo cha kuwaunganisha waafrika iliyojulikana kama jumuiya ya umoja wa Afrika (Organisation of Africa unity) mwezi wa 5 mwaka 1963.
UMOJA WA AFRIKA( AFRICA UNION).
Umoja huu uliundwa mwezi wa 5 mwaka 1963 na nchi huru za Afrika na apo awali ulijulikana kama jumuiya ya nchi huru za Afrika yani Oganaisation of Africa unity. Dhumuni lake ilikuwa kama chombo kikuu cha kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kisiasa kiuchumi na kitamaduni. Pia malengo ya awali ilikuwa ni kuisaidia Afrika kupambana na "ukoloni mkongwe" na "ukoloni mambo leo" pamoja na ubaguzi wa rangi na unyonyaji wa kibinadamu.
Katika misingi hiyo umoja huo wa nchi huru uliunda kamati ya ukombozi wa bara la Afrika (Pan African liberation and front line moverment) ambayo makao makuu yake yaliwekwa Dar es salam nchini Tanzania. Kazi kubwa ya kamati hiyo ilikuwa ni kuvisaidia vyama vya ukombozi kifedha,siraha na mbinu za mapambano na kazi hiyo ilifanyika kwa kutoa msaada mkubwa kwa vyama kama MPLA cha Angola, FRELIMO ya Msumbiji, ZANU ya Zimbabwe, ANC ya Afrika ya kusini na vingine vingi.
CHIMBUKO LA UMOJA WA AFRIKA.
Chimbuko la jumuiya hii ilianza kwa namana tatu(3) yani mpaka kufika kuundwa kwake imepitia katika hatua tatu zenye historia ya pekee kabisa.
Pamoja na hatua hiyo ikumbukwe kuwa asili ya umoja wa nchi huru ni kutokana na kile kinachoitwa "mageuzi ya kimitazamo juu ya ukombozi" (Plight of Pan African nationalist awareness) kutoka kwa viongozi wetu wa mwanzoni huko Amerika ya kaskazini, Amerika ya kati na Amerika ya kusini kwa watu kama William Du Boiss, Marcus Garvey na Washington pia mawazo yao yalipo kuwa kipeuo kwa kiwango kikubwa yaliathili mpaka viongozi wa kiafrika wa zama hizo amboa kalibu wengi wao walikuwa masomoni huku ughaibuni na pale walipo ludi nyumbani Africa nje na mawazo ya ukombozi pia waliona ni maana zaidi kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuwa na "sauti ya pamoja" viongozi hao kama Kwame Nkrumah wa Ghana, Sekou Touré wa Guinea.
Kwa msingi huu sasa Labda tuangalie namana ya jumuiya hii ilivyo anza "vichwani mwa watu wachache na mpaka hatimaye kuja kuwa wazo lililotekelezwa na kudumu mpaka leo". Na sisi tukiliishi mpaka leo pamoja na kuwa na changamoto tunazoziona leo. Kama nilivyo sema hapo mwanzo jumuiya hii imekuwepo kutokana na kile kilichoitwa "mageuzi ya kimitazamo ya ukombozi" kwa kupitia safari nyingi za kiharakati zilizo kuwa na changamoto na mivutano mikubwa kwa namna moja au nyingine toka mwazo mwa "vuguvugu la watu wenye asili ya Afrika" (Pan Africanism) huko nga'mbo ya bara la Afrika.
SEHEMU I
Vuguvugu la kwanza la "vuguvugu la watu wenye asili ya Afrika" (pan Africanism).
Ebu tuangalie kwa undani ni namna gani Vuguvugu hili kwa pana kabisa na kwa kiwango gani lilichangia kuwepo kwa jumuia ya nchi huru za Afrika. Kimsingi vuguvugu hili lilianzia huko bara la Amerika ya kaskazini na kusini miaka ya 1920 kwa kuundwa umoja wa watu weusi (universal negro improvement) chini ya Rais wake wa Marcus Garvey ambaye hata hivyo Garvey hakuwa kuizuru bala la Afrika kabisa na alikiwa mzaliwa wa Jamaika. Katika halakati za kuleta ushilikiano huu wqlijitokeza viongozi kadhaa kama Booker, william Du Bois, Washington na Marcus Garvey ambao waliweka misingi ya umoja ya watu weusi. Hatimaye umoja huu ulishika kasi na kuwa chimbuko la umoja wa nchi huru za Afrika baadae.
Ikumbukwe juhudi hizi zilianza kuonekana mwaka 1945 katika mkutano wa Manchester huko Uingereza. Katka mkutano huu viongozi wengi wa kiharakati kutoka marekani ya kaskazini na kusini na karibeani pamoja na Afrika walihudhuria. Badhi ya viongozi kutoka Afrika waliopata bahati ya kuhudhuria ni pamoja na Jomo Kenyatta wa Kenya, Kwame Nkrumah wa Ghana, kamuzu Banda wa Malawi, Saad Zaghur wa Egypt, Ahmed Ben Bella wa Argeria, John Dube wa Afrika ya kusini, Dr Benjamin Nandi Azikiwe wa Nigeria na Ahmed Ohdujo wa Kamerooni. Katika mkutano huu ndipo kulipo asisiwa mawazo ya ukombozi na umoja wa mtu mweusi na Afrika. Toka kipindi hicho fikra za waafrika juu ya ukoloni zilibadilika hasa kwa vuongozi walio hudhuria kikao kile.
SEHEMU II
Fikra za Kwame Nkrumah kusaidia ukombozi na kuwaunganisha Waafrika kupitia kile kilichoitwa "mkutano mkuu wa waafrika wote"
Karika mkutano huu uliofanyika jijini Accra Ghana mwaka 1958 ulioandaliwa na Kwame Nkrumah kutokana na kuhamasika na mkutano wa *Manchester pan Africanism conference* huko Uingereza uliochochoe hamasa za kuwaunganisha waafrika na kendeleza ukombozi dhidi ya mabeberu.
Katika mkutano huo Kwame Nkrumah aliwaalika viongozi mbalimabali wa vyama vya UKOMBOZI vilivyo kuwa vimeanzishwa kwenye nchi zao kwa harakati za kudai uhuru. Katika mkutano huu kulipangwa mikakatiti ya kuwaamsha viongozi na kuwapa dhana ya uzalendo wa ukombozi kwa nchi zao pia kupitia mkutano huu baadhi ya viongozi walibadilika kifikra na walipo ludi katika nchi zao walikuwa na miatazamo mipya ya mapambano zidi ya ukoloni mfano wa hii ni huko Kongo Patrice lumumba alipo ludi kutoka Ghana alikuwa na hamasa kubwa ya kukiimalisha chama chake cha MNC kwa misingi ya kitaifa na kufanikisha kujikomboa mwaka 1960. Hali hiyo pia ilionekana huko South Rhoedesia(zimbabwe) watu kama wakina Nkumbula,Sothe,Banana na Mugabe walipo ludi walikuwa na mitazamo mipya ya kupambana na utawala wa kilowezi hali iliopelekea wakina Mugabe kujiondoa kwenye chama cha ZAPU na kuanzisha chama cha ZANU ambacho kiliona njia ya mapambano ya mssituni ndio njia ya muafaka kwa ukombozi nchini Zimbabwe. Na hivyo ndiyo ilivyo kuwa kote balani Africa. Pia mkutano huu ajenda ya muungano wa Afrika ilichukua nafasi na walikubaliana kwanza kabla ya kuwepo kwa muungano ni vyema kushugurikia mapambano ya ukombozi kwanza amabayo ikiwa yatafanikiwa basi yatalahisisha umoja huo wa Afrika. Na katika juhudi hizo waliunda chombo maalumu cha kusaidia ukombozi ambacho baadae kilijulikana kama "kamati maalumu ya ukombozi wa afrika".
Hapa sasa ndo tunaona fikra ya Kwame Nkrumah *"..........Afrika ni lazima iungane"* ilipoanza kupenyeza na kuwa wazo lililo pevuka kwa kalibu kila kiongozi kwa wakati huu na baadae kuzaliwa kwa jumuiya ya nchi huru za Afrika (OAU). Je ni kwa namna gani wazo la Nkrumah lilikuwa zalio la umoja wa Africa? Na ni kwa namna gani wazo hilo liliwaathili viongozi wengine na kuwa chachu ya uzalendo wa Afrika? Ebu sasa tutazame kwa kina maswali haya katika sehemu ya tatu ya mapinduzi ya umoja huu........
SEHEMU III
Kujikomboa kwa Afrika kutoka kwenye ubeberu na kuundwa kwa jumuiya yenyewe
Mwaka 1960 hutajwa kuwa ni mwaka wa ukombozi barani Afrika kwani ndi mwaka ambao karibu nchi nyingi Africa zilijipatia uhuru wao kutoka kwa makoloni yao. Pia mwaka huo utazamwa duniani kama mwaka wa mabadilko ya ukombozi duniani kwani ndio mwaka Uingereza kwa mara ya kwanza walimchagua wazili mkuu wa kwanza mwanamke katika historia yao yani Magreth Sacher. Huko MAREKANI ilipitishwa sheria ya kupinga ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi na ndipo mpigania haki maarufu duniani Martin Luthet King aliuwawa na wahafidhina wasio penda mabadiliko hayo. Lakin kwingineko duniani China ilipata kiti cha kudumu cha balaza la usalama *umoja wa mataifa* wakati iliokuwa Muungano wa Kisovieti (USSR) ikimpeleka mtafiti wake huko mwezini.
Mwaka huu sio haba hata kidogo kwani hata Afrika kulianzishwa wazo la kuundwa Muungano wa umoja katika Afrika ambao ulichukuwa sura nyingi sana katka namana ya kufikiwa kwa maudhui yake.
JE NI NAMNA GANI WAZO LA KWAME NKRUMAH LILIVYO ZAA UMOJA HUO?
Muungano wa Madola ya Afrika ni wazo lililopendekezwa kwa ajili ya shirikisho la baadhi ya nchi zote huru 54 za katika bara la Afrika . Wazo hili linatokana na shairi la *Marcus Garvey* la mwaka wa 1924, Hail, United States of Africa . Na baadae kuchogezwa na Kwame Nkrumah katika kuundwa umoja huu ambao uliundwa mwaka 1963. Nini mitazamo ya *KWAME NKRUMAH* NA *MWL JURIAS NYERERE* juu ya kuundwa kwa shilikisho la kisasa la Afrika (united state of Africa)? Katika umoja huu?
Kama nilivyo eleza mwanzo sasa ebu tuone sasa mchago wa mwal nyerere na Nkrumah katiaka Harakati zao katika kuundwa kwa umoja wa Afrika zilianzia nje ya Afrika kwa kuwapigania Waafrika walioteswa kama watumwa hasa Marekani, zikaenea hadi Afrika ambapo mkutano wa kwanza ulifanyikia Ghana katika mji mkuu wake wa Accra. Mara tu baada ya Ghana kupata uhuru mwaka 1957, mwaka 1958 rais wa Ghana Kwame Nkrumah alitoa wazo la kuunda umoja wa Afrika.
Baada ya mazungumzo marefu wazo hilo lilikubaliwa na viongozi wa nchi huru za Afrika akiwemo *Mwalimu Julius Kambarage Nyerere* wa Tanzania. Hivyo basi umoja wa Afrika OAU ambao sasa unaitwa AU uliundwa mwaka 1963 nchini Ethiopia iliyokuwa nchi ya pekee ya Afrika ambayo ilifaulu kujitetea dhidi ya uenezaji wa ukoloni katika karne ya 19. Addis Ababa ndipo makao makuu yake yalipo pendekezwa na kukubalika pawe makao makuu Nyerere na Nkrumah walifikiri zaidi ni kwa vipi bara la Afrika lingeungana. Hapo ndipo kulipo anza utafauti wa kifikra juu ya namna gani Afrika iungane na kukatokea mitazamo miwili juu ya aina ipi ya muungano inayofaa kutumiwa kuufanikisha muungano wa shilikisho la Afrika.
*Sasa ebu tuanze kutazama Msimamo wa Nyerere*
Nyerere na mwenzake wa kongo Brazaville Filbert Youlou na kikundi cha Monrovia walitaka hatua hizo za kutengeneza nchi moja ya Afrika zisiharakishwe. Nyerere alitoa mawazo ambayo kwake yeye aliona yasingeruhusu muungano wa haraka kama alivyotaka kwame Nkrumah.
Alisema kila nchi inayo haki ya kutengeneza uchumi na siasa yake ili kuifanya nchi hiyo kutambulika, lugha na tamaduni zake pia zingestahili kutambulisha nchi hizo. Hivyo basi alisema ni vigumu kuwaunganisha watu wenye tamaduni tofauti, lazima kwanza tofauti hizo za kitamaduni ziondolewe kwanza kwa kuunda mashilikisho madogo ya kati ya nchi na nchi kwanza ndipo tuje kwenye shilikisho kubwa la Afrika, kitu ambacho kilihitaji muda zaidi.
Pia alisema matatizo mbalimbali yanayo zikumba nchi za Afrika, yakiwemo umaskini, vita vya wenyewe kwa wenyewe, ujinga na magonjwa mbalimali, pia njia tofauti tofauti za utawala wa viongozi vingekuwa vikwazo kikubwa cha kuunda umoja huo.
Nyerere alitoa wazo la kuunda mashirika mbalimbali yanayo ziunganisha nchi za Afrika kwanza kama hatua mojawapo ya kuelekea kuunda Afrika moja, hivyo mashirika kama vile SADC, ECOWAS,COMESA, EAC yaundwe kwanza kuimarisha umoja na utengano wazo hilo baadae lilionekan kuwa na maana kwani mashilika hayo na kadhalika yaliundwa.
*Lakini pia upande mwingine kulikiwa na mtazamo na Msimamo wa Nkrumah*
Naye Nkrumah alikuwa na mawazo kadha wa kadha ambayo kwa kiasi fulani yalitofautiana na yale ya Nyerere kama vile: Nkrumah na wenzake kutoka nchi za Mali chini ya Madibo Keita, Nigeria chini ya Benjamin Nandi Azikiwe, na Guinea chini ya Sekou Touré walitaka kuharakishwa kwa umoja huo, vinginevyo waliona kuwa ni kupoteza muda.
Nkrumah alisema haya kwa vigezo vifuatavyo: Kuundwa kwa umoja wa Afrika hakuwezi kuzifanya nchi zikose uhuru bali itasaidia kuleta muungano baina ya Waafrika wenyewe. Pia aliendelea kusema tatizo la tamaduni tofauti halikustahili kukwamisha harakati za kuunda umoja wa Afrika kwani kuendelea kuchelewa kungetoa nafasi kwa wakoloni kurudi kuitawala Afrika kwa urahisi, hivyo umoja ulikuwa njia pekee ya kuwazuia wakoloni kutawala tena na hayo matatizo mengine mengi yangeendelea kutatuliwa huku umoja ukiwa umeshaundwa.
Nkrumah pia alisema muungano wa Afrika ungesababisha kujenga nchi huru na imara yenye kusimamia maamuzi yake kuhusu uzalishaji katika kilimo na bei katika soko la dunia ambayo ilimilikiwa na kupangwa na mabepari.
Kwa kuangalia na kutathmini mawazo hayo, viongozi hao walionekana kuwa chumvi ya Afrika kwa msaada wao katitika kujenga na kuleta uhuru miongoni mwa nchi za Afrika.
Utafauti huu ndio uliokwamisha ndoto ya mwanzoni ya kuwa na Dola moja Africa. Pamoja na mivutano hiyo bado wazo la kuungana limekuwa likiendelea toka kipindi hicho mpaka sasa kwani hata Kiongozi wa zamani wa Libya Muammar al-Gaddafi , ambaye 2009 alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA), aliendeleza wazo la Muungano wa Madola ya Afrika katika mikutano mwili ya kanda ya Afrika: wa kwanza mwezi Juni 2007 mjini Conakry, Guinea, halafu tena mnamo mwezi wa Februari mwaka 2009 mjini Addis Ababa, Ethiopia. Gaddafi awali alisukuma kuanzishwa kwa suala hili katika mkutano uliofanyika mwaka 2000 mjini Lomé, Togo, aliealeza UA kama kushindwa kwa baadhi ya mambo; Gaddafi alidai ya kwamba muungano wa kweli pekee ni Muungano wa kuwa na shilikisho la kisiasa na ndiyo unaweza kutupatia uthabiti na utajiri kwa Afrika yetu.
Baadhi ya viongozi wakuu wa UA walikubaliana na shirikisho lililopendekezwa, wakiamini ya kwamba ingeliweza kuleta amani katika Afrika mpya.
Alpha Oumar Konaré , Rais wa zamani wa Mali na mwenyekiti wa zamani wa
Tume ya Umoja wa Afrika , alizungumzia wazo hili katika sherehe za Siku ya Afrika , mnamo Mei 25, 2006 Tena kama sehemu ya kuiunganisha Afrika
Kwa kuhitimisha, tu japo sio kwa umuhimu wake bado wazo la kuifanya Afrika kuunda umoja wa nchi moja ungali unaishi mpaka leo toka ulipo asisiwa na viongozi hao yani Nkrumah, Nyerere na wengineo kama vile Jomo Kenyatta wa Kenya, na Nelson Mandela wa Afrika Kusini ni miongoni mwa viongozi wa Afrika wanaostahili kukumbukwa kwa mchango wao mkubwa katika kupigania uhuru wa Afrika.
Pamoja na kushindikana kwa shilikisho la kisiasa la Afrika bado umoja wa Afrika unaendelea kuwa hai na ikumbukwe tu kwamba Umoja wa Afrika (UA) (kwa Kiingereza African Union) (AU) ; (Kifaransa : Union Africaine) (UA) ; (Kihispania : Unión Africana) (UA) ; Kireno: (União Africana) (UA) ni muungano wa nchi 54 za Afrika ulioanzishwa mnamo Julai 2002 . Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo 1963 hadi 2002. Nia ya umoja huu bado ni iliile kama ya madhumuni ya mwanzo ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na
1- bunge moja,
2-benki moja,
3- jeshi moja,
4- rais mmoja,
5-sarafu moja, n.k.
Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile
1-vita ,
2-njaa ,
3-Ukimwi , n.k.
Nchi wanachama
Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 53. Laini mpaka mwaka 2011 *Sudani kusin* iiliongezeka na kuwa mwanachama wa 54 Ndizo nchi karibu zote za bara la Afrika isipokuwa Moroko iliyoondoka mwaka 1985 kwa sababu UA ilitambua
Sahara ya Magharibi kuwa nchi ya kujitegema wakati Moroko inadai ya kwamba ni eneo la majimbo yake ya kusini. Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini mwaka 2002. Na Mikutano mikuu ya UA ni kama ifuatavyo.....
1. Durban (Afrika Kusini): 9-11 Jul. 2002.
2. Maputo (Msumbiji): 10-11 Jul. 2003.
3. Sirte (Libya), mkutano wa dharura: Feb. 2004.
4. Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Jul. 2004.
5. Abuja (Nigeria): 24-31 Jan. 2005.
6. Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Jul. 2005.
7. Khartoum (Sudan): 16-24 Jan. 2006.
Na Viongozi wake toka mwaka 2002 ni kama ifuatavyo........
1-Thabo Mbeki 9 July 2002 -10 July 2003 South Africa
2-Joaquim Chissano 10 July 2003 -6 July 2004 Mozambique
3-Olusegun Obasanjo 6 July 2004 -24 January 2006 Nigeria
4-Denis Sassou-Nguesso 24 January 2006 -24 January 2007 Republic of the Congo
5-John Kufuor 30 January 2007 -31 January 2008 Ghana
6-Jakaya Kikwete 31 January 2008 -2 February 2009 Tanzania
7-Muammar al-Gaddafi 2 February 2009- 31 January 2010 Libyan Arab Jamahiriya
8-Bingu wa Mutharika 31 January 2010 -31 January 2011 Malawi
9-Teodoro Obiang Nguema Mbasogo 31 January 2011 -29 January 2012 Equatorial Guinea
10-Yayi Boni 29 January 2012- 27 January 2013 Benin
11-Hailemariam Desalegn 27 January 2013- 30 January 2014 Ethiopia
12-Mohamed Ould Abdel Aziz 30 January 2014 -30 january 2015 Mauritania
13- Robert Mugabe 30 january 2015-30 january 2016.
14-Idriss Deby 30 january 2016 mpaka sasa.
Rais wa Chad Idriss Deby amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, akichukuwa nafasi ya rais wa Zimbabwe Robert Mugabe. Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika Rais Idriss Deby wa Chad ambaye Uteuzi wake huo umefanyika wakati viongozi wa Afrika walipokutana Jumamosi (30.01.2016) katika juhudi za kukomesha mizozo yenye kuhusisha matumizi ya silaha ukiwemo ule wa Burundi ambapo walipiga kura isio na kifani ya kutuma wanajeshi wa kulinda amani nchini humo licha ya upinzani mkali wa nchi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni *Nikozana Dlamini-Zuma*
Spika wa Bunge la Umoja wa Afrika ni
*Bethel Nnaeme*.
MWISHO
pamoja na changamoto nyingi inazo kumbana nazo AU imeendelea kuwa na mapambano ya kuisuka Africa mpya ambayo iliishi kwenye ndoto za *Kwame Nkrumah* na *Mwalimu Nyerere*.
*"Mungu ibariki Afrika, Mungu bariki waafrika, Mungu bariki Fikra za waafrika"*