Zimbabwe ni moja ya nchi inayopatikana katika bara la Afrika. Katika bara la Afrika nchi ya Zimbabwe inapatikana upande wa kusini. Nchi ya Zimbabwe inapakana na nchi kama, Msumbiji kwa upande wa kaskazini-mashariki na kusini-mashariki, nchi ya Zambia kwa upande wa kaskazini-magharibi, nchi ya Botswana kwa upande wa kusini-magharibi na nchi ya Afrika kusini kwa upande wa kusini. Nchi ya Zimbabwe ina ukubwa wa maili za mraba 242,700 , sawa na kilomita za eneo 390, 580. Mji mkuu wa Zimbabwe unaitwa Harare. Kihistoria nchi ya Zimbabwe ilitawaliwa na Mwingereza kuanzia miaka ya 1890 na mpaka kufikia miaka ya 1965 harakati za kudai Uhuru zilianza zikiongozwa . Na mpaka kufikia miaka ya 1980 nchi ya Zimbabwe ilipata uhuru. Makabila makuu ya Zimbabwe ni Washona na Wandebele. Wakazi wa kwanza katika ardhi ya Zimbabwe walikuwa Wakhoisani waliokuwa wakiishi maporini miaka mingi kabla ya kuja kwa Wabantu. Wakhoisani walipata kuishi hapo na ushahidi ulipatikana kwa kukuta aina za nyumba ambazo hujengwa na watu wa kabila la Wakhoisani. Na kutokana na ujio wa makabila ya Wabantu, Wakhoisani walifukuzwa na wangine kuchangamana na makabila ya kibantu. Ukweli ni kwamba kulikuwa na makabila mengi yaliyokuwa yakiishi hapo mara baada ya kuwafukuza Wakhoisani. Lakini mpaka wageni wanafika kwa mfano Wareno, Wadachi na Waingereza walikuta makabila wawili ambayo ni Washona na Wandebele. Washona na wandebele walikuwa na miji yao ilikuwa imejengeka sana kwa majumba makubwa yaliyojengwa kwa mawe. Na hivyo mpaka ukoloni unaanzishwa kulikuwa na makabila mawili na yalipigana sana kwenye vita vya Washona na Wandebele kwa lengo la kupinga ukoloni. Asili ya neno Zimbabwe linatokana na kugundulika kwa jumba la mawe lililofahamika kama Zimbabwe kubw(Great Zimbabwe). Kabla ya nchi hii kuitwa Zimbabwe ilikuwa ikiitwa Rhodeshia ya Kusini (Southern Rhodesia) na baadae kuitwa Zimbabwe ya Rhodesia( Zimbambwe of Rhodesia) . Lakini kutokana na ugunduzi wa jumba lililojengwa kwa mawe lililopata kujengwa miaka mingi tangu miaka ya 1000-1400. Jengo hilo lilijengwa na Washona waliokuwa wakimiliki teknolojia ya ujenzi wa majimba kwa mawe. Jengo hilo liliitwa kwa jina la kishona Dzimba Dza Mabwe. Na mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo miaka ya 1980, waliamua kuita nchio hiyo Zimbabwe kwa lengo la kurinda heshima ya nchi. Ukweli ni kwamba jengo hilo liligunduliwa na mwanajiolojia kutoka Ujerumani mnamo miaka ya 1871, alifahamika kwa jina la Carl Mauch. Raisi wa kwanza wa zimbwabwe alikuwa Caanaam Banana(1936-2003) Aliyepata kutawala nchi hiyo chini ya chama cha ZANU(Zimbabwe African National Union) kuanzia miaka ya 1980-1987. Wakati huo Robert Mugabe akiwa kama waziri mkuu. Na raisi wa sasa ni Robert Mugabe (1924- ) kuanzia miaka ya (1987-sasa) chini ya Chama cha ZANU-PF(Zimbabwe African National Union-Patriotic Front). KARIBU Zimbabwe.
Taswira inaweza kujumuisha: nyasi, mti, mmea, anga, nje na asili