Unafiki Wa Wakomeshaji Wa Biashara Ya Watumwa

Image result for biashara YA UTUMWA

Kama mtu yeyote anataka kudhani kwamba sababu ya kukomeshwa kwa utumwa ni maendeleo ya unyofu wa maadili, basi anashauriwa kuangalia msimamo wa watu waliokuwa wanashughulikia suala la kukomesha biashara ya watumwa katika mfumo wa malengo yao ya kiuchumi. Hivyo tunaona kwamba wale wale washikiliaji wa maslahi ya West Indies ambao kabla ya tatizo lililotajwa, walikuwa ni waungaji mkono motomoto wa biashara ya watumwa sasa waligeuka kuwa “waungwana wenye huruma na shauku ya kuukomesha utumwa”. Dk. Williams anasema, kwa kejeli kabisa, ilikuwa ni wamiliki wa watumwa wa siku za nyuma wa West Indies ambao sasa walishikilia tochi ya kuwahurumia binadamu.
Wale ambao, katika mwaka wa 1807, kwa majonzi walikuwa wanatabiri kwamba kukomesha biashara ya watumwa ya Uingereza “ingesababisha kupungua kwa biashara, kupungua kwa ushuru wa kodi, na kupungua kwa safari za baharini; na hatimaye kudhoofisha na kuondoa kabisa msingi mkuu wa ustawi wa Uingereza, walikuwa, baada ya 1807, watu wale wale waliokataa ‘mpango wa mtu’ kuwaiba watu masikini na ambao hawana jinsi ya kujitetea.”
Manufaa ya West India katika mwaka wa 1830 yaliweka azimio la “kuchukua hatua madhubuti zaidi kusitisha biashara ya watumwa ya nje; kushughulikia suala la ukan- damizaji uliokwisha fanywa ambao kwamba ustawi wa makoloni ya Uingereza ya West Indes… hatimaye yali- utegemea. Wajumbe kutoka Jamaica, walopelekwa Uingereza mwaka 1823, walitangaza kwamba makoloni yangepatanishwa kwa urahisi kuhusu kukomeshwa kwa biashara ya kishenzi na ya kinyama, ambayo ustaarabu ulioendelea wa wakati huu hukuiruhusu tena kuwepo… Kundi kubwa la kukomesha biashara ya watumwa lilijidhihirisha nchini Jamaica katika mwaka 1849.
Auj claplo, vyama na madhehebu viliunganishwa kuhusu suala la Africa kutendewa haki. Walilaani biashara ya watumwa na utumwa kama ni “kinyume cha ubinadamu iliyozalisha maovu mabaya sana Afrika - kuwadhalilisha wote waliohusika katika biashara hiyo, na kudhuru maadili na utashi wa kiroho wa watumwa, na kusihi kwamba neno la kuchuk- iza ‘mtumwa’ liondolewe kwenye msamiati duniani pote. UTUMWA LAZIMA UANGUKE, na utakapoanguka, JAMAICA ITASTAWI! Walitamka kwa ukali, iliingia kwenye vita nyingi bila ya sababu zilizo halali.” 1
Na palikuwepo na manufaa gani ya vifungu vya maneno vilivyo vikali na ambavyo vinaweza kuamuliwa kutokana na ukweli kwamba ubepari wa Uingereza, hata baada ya kuvuruga utumwa wa West Indian, “Uliendelea kustawi kutokana na utumwa uliokuwa unaendelea huko Brazil, Cuba na utumwa wa Amerika ya Kaskazini na Kusini.” Kwa hiyo, kwa maneno ya Profesa Brogan, “tunapata mafumbo ya wajibu uliogeuzwa. Ilikuwa sawa kabisa kwa watetezi wa hoja ya kukomeshwa utumwa, kulaani matumizi ya sukari iliyo zalishwa na watumwa kutoka West Indes, lakini hakuna aliyependekeza kusimamisha matumizi ya pamba iliyozalishwa kutoka Marekani (U.S.A.). Hakika, hakuna mtu aliyependekeza kwa dhati kuacha kutumia sukari iliyozalishwa na watumwa kutoka Brazil au Cuba. Fedha sio hisia, hisia za uovu za uzuri, husokota na kupotosha njama.”
Dk. Williams anaandika, “Baada ya India, Brazil na Cuba, bila ya dhana yoyote. Je, muungwana yeyote angeweza kuhalalisha pendekezo lolote lililopangwa kuimarisha minyororo ya utumwa ambayo bado imewafunga Watu Weusi wa Brazil na Cuba. Kwa usahihi hiyo ndio ilikuwa maana ya biashara huru ya sukari.
Kwani baada ya mwaka 1807 British West Indians walikataliwa na kunyimwa kuendesha biashara ya watumwa, na baada ya 1833 wakanyimwa nguvu kazi ya watumwa. Kama watetezi wa kukomesha utumwa walipendekeza sukari ya kutoka India, kwa makosa, kwa misingi ya ubinadamu kwamba ni sukari iliyolimwa na watumwa huru, ilikuwa ni wajibu wao kwa kanuni zao na dini yao kususia sukari iliyolimwa na watu wa Brazil na Cuba. Katika kuanguka kufanya hivi isiamuliwe kwamba hawakuwa sahihi, lakini si jambo la kukanusha kwamba kushindwa kwao kutumia njia hiyo ilivuruga hoja ya ubinadamu. Baada ya 1833, watetezi wa kukomesha utumwa, waliendelea kumpinga mkulima wa West Indian ambaye sasa aliajiri wafanya kazi huru. Ambapo, kabla ya hapo 1833, waliwagomea wamiliki wa watumwa wa Uingereza, baada ya 1833 waliunga mkono sababu ya wamiliki wa watumwa wa Brazil.”2
Kuondolewa kwa Watu Weusi kishenzi kutoka Afrika ni shughuli iliyoendelea kwa karibu miaka 25 tangu 1833, ambao walipelekwa kwenye mashamba ya miwa ya Brazil na Cuba. Uchumi wa Brazil na Cuba ulitegemea biashara ya watumwa. Msisitizo peke yake ulidai kwamba watetezi wa kukomesha utumwa wa Uingereza walipinga biashara hii. Lakini jambo hilo lingerudisha nyuma maendeleo ya Brazil na Cuba na matokeo yake kuzuia biashara ya Uingereza. Haja ya kupata sukari ya gharama ya chini baada ya 1833 ilishinda chuki yote ya utumwa. Tishio ambalo hapo mwan- zo lilichochewa na fikira ya mswaga watumwa wa Uingereza wa West Indies mwenye mjeledi; mswaga watumwa wa Cuba mwenye mjeledi, panga, jambia,. kisu na bastola na kufuatwa na mbwa mwitu, haikuamsha hata maoni ya watetezi wa kuzuia biashara ya watumwa.”3
Hivyo ni wazi kwamba sababu halisi yaubinadamu na uungwana wa Uingereza wala haikuwa usawa wa kiunyofu au mwamko wa kimaadili bali ilikuwa ni kwa sababu ya shinikizo la kiuchumi na kuwaumiza washindani wao wa biashara. Kwa maneno ya Profesa Brogan, somo la Ubepari na Utumwa linavunja moyo na kufadhaisha kama si jipya. “Pale ilipo hazina yako ndipo moyo wako unapo lala.’

Post a Comment

0 Comments